Hillary Clinton afunguliwa kesi kwa mauaji ya Libya 2012
Wazazi wa wamarekani wawili waliouliwa miaka minne iliyopita nchini Libya wanamshutumu mgombea Urais kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton, kwa kuchangia kutokea kwa mauaji hayo.
Clinton waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani kipindi ubalozi wa Marekani nchini Libya uliposhambuliwa.
Patricia Smith na Charles Woods, ambao ni wazazi wa Sean Smith na Tyrone Wood wamesema kuwa matumizi ya barua pepe binafsi zilichangia mauaji ya watoto wao.
Msemaji wa kampeni za Hilary Clinton amepinga tuhuma hizo. Ingawa kamati ya Chama cha Republican inaweka wazi mabaya aliyoyatenda Hilary, jambo linalo tia doa kampeni zake za Urais.
Uvamizi wa majeshi ya kiislam katika ubalozi wa Marekani uliwauwa raia wanne wa nchi hiyo akiwemo Balozi Chris Stevens.
No comments:
Post a Comment