Alisema serikali haipo tayari kuona mtu yeyote anaachwa nyuma katika utekelezaji wa maendeleo endelevu na kwamba kila mtu anajukumu la kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii ili kukuza uchumi wa nchi na kwamba wamejipanga kutoa elimu kwa wote hususan ujasiriamali.
Hata hivyo alizungumzia changamoto zilizopo ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto na kwamba jamii iwe tayari kukemea hilo kwani maendeleo hayatafikiwa ikiwa masuala hayo yataendelea.
“Hatuwezi kufika mbali ikiwa hakuna usawa wa kijinsia,takwimu znaonyesha watoto wengi wanashindwa kumaliza masomo kutokana na unyanyaswaji pamoja na mimba wakiwa shuleni, lazima kila mwanajamii akemee vitendo hivi ili tufikekie maendeleo endelevu.” Alisema.
Alisema mikakati ya kufikia maendeleo endelevu yameanza ambapo sera mbalimbali zimeshatungwa ikiwemo kupinga ukatili,utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari pamoja na uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi kwa kuwaweka karibu a taasisi za kifedha.
Kwa upande wao wawakilishi wa umoja wa mataifa walisema wapo tayari kuisaidia Tanzania katika kupambana kufikia maendeleo endelevu huku wakiyaomba makundi maalum kuwa karibu na ofisi zao ili kutatua janga la umasikini.
Akizungumza katika kongamano hilo, Amon Manyama ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa progamu ya maendeleo endelevu, alisema katika kutekeleza ahadi za kufikia maendeleo endelevu, wanataoa kipaumbele kwa makundi maalum na kwamba wapo tayari kukaa nao meza moja kujadili changamoto zao.
Alisema kila mtu anahaki ya kupata haki za kibinadamu na hivyo kutokana na makundi hayo kusahaulika wameamua kuwapa kipaumbele ili yapate haki zao za msingi ikiwemo kuwa na maisha bora na kukua kiuchumi.
“Kutokana makundi haya yamesahaulika kwa siku nyingi, tunatoa kipaumbele kwao na tunawakaribisha katiaka ofisi zetu, tukae, tujue changamoto zinazowakabili pamoja na kuzitatua, tunataka kuhakikisha makundi maalum yanaopata haki za msingi.” Alisema Manyama.
Malengo 17 yaliyoekwa na Umoja wa Mataifa katika kufikia maendeleo endelevu hadi kufikia 2030 ni pamoja na kuondoa umasikini, kuwepo kwa usawa na kupata haki zote za kibinadamu
No comments:
Post a Comment