:
Kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamni ya Chama dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mtungi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Lipumba na wenzake imeendelea leo ambapo Jaji Kihiyo amekubaliana na hoja za Mawakili wetu wasomi Mhe. Daimu Halfani na Juma Nassor juu ya kupatiwa dokoments zilizoombwa kwake kwa ajili ya CUF kuomba kufanyika kwa REVISION ktk Mahakama Kuu ya Rufaa Tanzania kutokana na maamuzi (Ruling) ya Jaji Kihiyo Kukataa kujitoa kuendelea kusikiliza kesi hiyo yaliyowasilishwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF.
Kesi imepangwa kutajwa tena tarehe 22/3/2017.
Mara documents zilizoombwa (Ruling, Proceedings and Drawn Order ) zikiwa tayari na kukabidhiwa kwa mawakili wetu (CUF) shauri hilo halitaendelea kusikilizwa mbele ya Jaji Kihiyo mpaka Mahakama Kuu ya Rufaa itakaposikiliza na kutoa uamuzi juu ya maombi ya mapitio (Application for Revision) yatakayo wasilishwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF kuamuliwa.
Haki sawa kwa wote.
Maharagande.
No comments:
Post a Comment