• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 14 August 2017

    WAJUMBE WA BODI YA BARABARA WAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI MITATU YA BARABARA INAYOTEKELEZWA KATIKA MANISPAA YA UBUNGO

    Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
    Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa ni ziara ya kukagua miradi ya barabara
    inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Leo Agosti 14
    Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
    Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua daraja lililopo kwenye barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa ni ziara ya kukagua miradi ya barabara
    inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Leo Agosti 14
    Picha ya pamoja ya viongozi mbalimbali wakiwa na Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
    Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa ni ziara ya kukagua miradi ya barabara
    inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Leo Agosti 14
    Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo wakati wa ziara ya Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
    Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua barabara ya Watani kwa Jongo katika Kata ya Makurumla. Leo Agosti 14
    Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
    Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakimsikiliza kwa makini Mtaalamu wa Barabara akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa barabara ya Kifuru-Msigani wakati wa ziara ya kukagua miradi ya barabara
    inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Leo Agosti 14
    Muonekano wa Barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa katika hatua za awali za ujenzi.Leo Agosti 14
    Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
    Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo wamefanya ziara katika miradi ya barabara
    inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa lengo la kujua
    Maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.
    Miradi iliyotembelewa ni Barabara ya Watani kwa Jongo Kata
    ya Makurumla ambayo ina Urefu wa kilomita 1 na inajengwa kwa kiwango cha
    changarawe kwa kutumia fedha za Ndani (own source), Barabara ya Ubungo Msewe
    kutokea  Kimara Baruti yenye urefu wa
    Kilomita 2.6 inasimamiwa na TAN ROADS, Pia Barabara ya Kifuru – Msigani yenye
    urefu wa kilomita 4.0 ambayo ina simamiwa na TAN ROAD na inajengwa kwa kiwango
    cha lami.
    Wajumbe wa bodi ya Barabara hiyo wamedhamiria kuhakikisha
    miradi iliyopangwa  inatekelezwa kwa
    wakati na kwa ubora ili kuboresha miundo mbinu ambayo itawanufaisha na
    kuwaletea maendeleo wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
    Wajumbe hao kwa Upande wa Manispaa ya Ubungo ni Mhe. Mbunge
    wa viti maalumu Suzan Lymo, Mkururugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi
    Kayombo, Katibu tawala wa Wilaya Ndg James
    Mkumbo  na Wataalamu kutoka ofisi
    ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI