KATIKA
kusherekea kutimiza miaka miwili ya kiutendaji tangia achaguliwe kuwa
Diwani wa kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto, amefunguka mazito ikiwa
ni njia ya kwajibu wale wanaomrushia lawama kuhusiana na utendaji wake
wa kazi hususani kero ya Bara bara.
Akizungumza
na Waandishi wa habari l Kata ya Vingunguti CCM kwa Kombo Jijini Dar es
Salaam katika kutimiza miaka miwili ya kiutendaji , Diwani
Kumbilamoto, amesema kuingia kwake kwenye siasa ni kwa ajili ya
kuwatumikia Wananchi wanyonge waliompa heshima ya kushika kiti hicho na
sio kwa ajili ya kupiga dili ya kuwa nyonya waliomchagua .
Aidha,
Kumbilamoto, ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Wilaya ya Ilala,
amewataka wale wanasiasa wanaomchafua na kutaka kukuwagombanisha na
Wananchi wake waache mara moja kwani siasa hizo zinadidimiza maendeleo.
Kumbilamoto,
amefanya mkutano huo ikiwa ni njia ya kujitathimini utendaji wake
wa kazi na nguvu za usimamizi wa ilani ya Chama chake kilichompa ridhaa
ya kuwa Diwani katika kipindi cha miaka miwili, kujua dhamira ya Wana
Vingunguti na kuona ni wapi walipotoka, walipo na wapi wanatakiwa
kwenda.
"Ili
nchi iwe na maendeleo ni lazima viongozi waepuke kufanyakazi kwa mazoea
na kuweka siasa pembeni huku dhamira yao kuu ni kuweka vitendo mbele
katika kusukuma gurudumu la maendeleo, kama tutakuwa na siasa nyingi za
kuahidi au kupakazana matope maendeleo tunayoyataka tutayasikia kwa
wenzetu, nchi bado sana tupo nyuma tunatakiwa kupambana na kutumia
ubunifu wetu kusonga mbele".Amesema Kumbilamoto
Moja
ya matatizo ambayo Diwani Kumbi lamoto amekuwa akilalamikiwa ni pamoja
na suala la uchakavu wa miundombinu ya Bara bara ya Mnyamani na
Vingunguti, jamabo ambalo amesema halimuhusu kwamba bara bara zote zipo
chini ya Serikali kuu kupitia kwa TARURA zikisimamiwa na Waziri wa
Tamisemi Suleimani Jaffo.
Katika
changamoto hiyo, Diwani huyo amedai amekuwa akipokea vitisho na matusi
hadi kufikia kutukanwa mzazi wake kuhusiana na ubovu wa Bara bara jambo
ambalo limekuwa likimuuma sana na ameamua kulitolea ufumbuzi ili
kuepukana na maswali hayo yanayohusiasha mgongano wa kisiasa dhidi ya
Chama chake cha CUF.
Hata
hivyo, Kumbilamoto, amesema kuwa TARURA iliaznishwa kwa mujibu wa
kisheria kwamba ni chombo pekee kitakacho simamia miundombinu ya Bara
bara kuanzia ngazi za Vijini na Mjini ikiwa chini ya Serikali kuu ambapo
walikusudia kuimarisha miundombinu pamoja na kufanya maendeleo endelevu
ya bara bara.
Pia
amsema kama yeye ingekuwa ni kikwazo cha kutokutengenezwa ka bara bara
hiyo, basi angejiuzuru ila kwa vile haipo chini yake na hana jukumu hilo
yeye kazi yake ni kufanya ufuatiliaji na usimamizi ataendelea
kuwatumikia wananchi wake kwa kuwaaminisha kwa kile anachokifanya kwenye
kata yake bila ubaguzi na kwa vitendo zaidi.
Amewashukuru
baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto waishio katika kata yake kwa
ushirikiano mzuri wa kuwahabarisha watumiaji wengine kuhusu kero ya
bara bara huku pongezi kubwa zikienda kwa Wananchi wake kwa uvumilivu
wa mambo na ahadi ambazo ameziahidi na kufanyiwa kazi
"Nataka
kuwaambia sitotishika na mtu, nipo radhi kufa lakini nitasema ukweli
daima , Vingunguti siyo ya Kumbilamoto, ni ya wananchi wote na
maendeleo ya wana vingunguti ni ya wote, tupuuze wanasiasa wanaotaka
kutugombanisha tufanye kazi, tumechoshwa kula mlo mmoja kama kiboko
tunahitaji milo mingi zaidi".Ameongeza Kumbilamoto
Amewaomba
Sungungu kutumia busara katika malindo yao kwani kazi yao ni
kuhakikisha ulinzi na usalama na sio kupeleka maneno kutoka kwa familia
wakifanya hivyo watakuwa wagombanishi wakubwa na watatoka kinyume na
maadili ya kazi zao.
Naye
Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ilala, Bakari Shingo, amesema maendelo ya
Taifa huletwa na utendaji bora wa kazi, hivyo amewataka Viongozi kuacha
kupiga domo badala yake wafanye kazi kwa Vitendo kama anavyofanya
Kumbilamoto.
Mmmoja
ya wakazi wa Vingunguti, Hadija Shabani, amesema kero ya Ushuru mkubwa
wa ukusanyaji wa taka taka inayofika Shilingi 3000/= inawaumiza sana
huku kero hiyo ikionekana kuwa adha kwa wakazi wote waishio kata hiyo
ambapo Mh: Diwani Kumbilamoto ameahidi kukaa na kamati yake kuangalia
namna ya kutatua.
Miongoni
mwa mafanikio ambayo yameonekana kuteka nyoyo za Wakazi wa Vingunguti
ni pamoja na huduma za afya ambapo Zahanati ya Vingunguti haikuwa na
Ambulence lakini kwa sasa wamepatiwa, makusanyo ya juu ya pesa ya
Zahanati kutoka Shilingi Milioni 2 kwa 3 hadi kufikia milioni 8-9 kwa
mwezi, Mashine ya kufulia, Mashine ya presha na kisukari, tochi ya
uchunguzi wa tonsi pamoja na kutanua Maabara ya Zahanati ya Vingunguti,
kuboresha wodi za wazazi, kuwawekea TV Labour ambapo wazazi wamekuwa
wakifuatilia kinachoendelea duniani, kuongeza choo Zahanati ya
Vingunguti ambapo awali kulikuwa na choo kimoja ila kwa sasa vipo viwili
cha Madaktari na wauguzi pamoja na cha Wagonjwa, pamoja na kufunga
Friji nne jambao ambalo lilitaka kupoteza hadhi ya Zahanati hiyo ambayo
ilikuwa hatarini kufutwa kutokana na uchakavu wa miundombinu.
Katika
upande wa Vijana , amefanikiwa kuimarisha mahusiano mazuri ya Vijana
kuwakutanisha pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha maisha yao kwa
kuwakabidhi Boda boda kama kitega uchumi chao, kusaidia Jogging Klabu
zilizopo Vingunguti na michezo kwa ujumla.
Diwani Kumbilamoto (kulia), akikabidhi Boda boda kwa Vijana wake ikiwa ni ahadi yake kwa mafanikio ya Wana Vingunguti. |
Upande
wa Siasa amefanikiwa kutanua wigo mpana wa mawsiliano na kushirikiana
na Serikali kuu ukizingatia ni Naibu Meya mwenye dhamana ya kusimamia
maendeloa ya Ilala kwa kufuata kauli mbiu ya Rais Magufuli ya Maendeleo
hayana chama.
No comments:
Post a Comment