• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday 28 January 2017

    TAMASHA LA "MAJIMAJI FLAVA" LAFANA I

    Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Leah Kihimbi ambaye alimwakilisha Mhe. Waziri Nape Nnauye akitoa maoni yake kuhusiana na igizo la Tamasha la "MajiMaji Flava" ambalo lilionyesha baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na Wajerumani enzi za ukoloni dhidi ya watu weusi. Tamasha hilo lilifanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. 



    Waigizaji wa Tamasha la "MajiMaji Flava" wakielimisha jamii kwa vitendo juu ya baadhi ya matukio yaliyowahi kutokea wakati wa kipindi cha ukoloni wa Wajerumani nchini Tanzania 27/01/2017 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. 



    Baadhi ya wageni waalikwa toka mataifa mbalimbali wakishuhudia maigizo mbalimbali wakati wa Tamasha la "MajiMaji Flava" ambalo lilionyesha baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na Wajerumani enzi za ukoloni dhidi ya watu weusi. Tamasha hilo lilifanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. 

    Waigizaji kutoka Ujerumani na Tanzania wakitoa burudani ya muziki wakati wa "Tamasha la MajiMaji Flava" lililofanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM).

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI