• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday 28 January 2017

    DC Mjema apiga marufuku maroli kushusha mizigo mchana

    Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amepiga marufuku magari ya maroli kupakua mizigo muda wa mchana na badala yake wafanye hivyo majira ya usiku.
    Agizo la DC Mjema amelitoa kufuatia kuwepo kwa foleni kubwa wakati wa mchana inayosababishwa na malori na kupelekea baadhi ya shughuli  kutofanyika kwa wakati.
    Akitoa agizo hilo eneo la Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anafanya usafi na wafanyabiashara na wakazi wa eneo hilo  DC Mjema ameeleza kuwa Manispaa wataweka utaratibu wa sehemu ya kupaki Malori hayo kisha wale wenye baiskeli za matairi matatu maarufu kama Guta watakuwa wanaibeba mizigo hiyo na kuipeleka kwa wahusika.
    Katika hatua nyingine DC Mjema amewataka wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga waendelee kujiandikisha ili wapangiwe maeneo na kueleza kuwa mpaka sasa waliojiandikisha ni zaidi ya 2000, kujiandikisha huko kutawasaidia kutambulika na Serikali, Mamlaka ya Mapato (TRA ) halikadhalika Jeshi la Polisi Nchini, ambapo watapatiwa Vitambulisho maalum na meza zao za kufanyia biashara zitawekewa namba.
    Pia DC Mjema amewataka Machinga wanaofanya biashara maeneo ya barabara ya Mwendokasi wajiandikishe mapema na waondoke maeneo hayo kwa hiari kabla serikali haijachukuwa hatua stahiki kwani si salama, na kusisitiza kuwa mwenye malalamiko yeyote aende katika ofisi za wamachinga zilizopo mtaa wa Nyamwezi na Narung’ombe huku akihaidi kuwa Manispaa itawaletea vifaa vya ofisi ikiwemo viti, meza na kompyuta, na kusema kuwa mambo ya kukimbizana na machinga yawe ya kihistoria kila mmoja afanye biashara kwa weledi na kisasa kama wanavyofanya mataifa mengine.
    Aidha DC Mjema amewatoa hofu wafanyabiashara wa maduka kuwa wasione kwamba hawataweza kufanya biashara zao kwani serikali inaweka mpango maalum wa kufanyabiashara kati ya machinga na mfanyabishara mkubwa kwa kutofautisha uuzaji wa bidhaa eneo moja.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI