• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday 28 January 2017

    TAWJA: Wananchi wajitokeze kupata elimu ya Sheria

    Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) kimewataka watanzania wajitokeze kwa kutembelea mabanda yao yaliyopo Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa sasa ili waweze kujifunza masuala mbalimbali ya kisheria.
    Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Jaji Hanifa Mwingila ambaye ni mwanachama na hakimu ya anaetokea wilaya ya Kinondoni, katika kuadhimisha wiki ya sheria ambapo kilele chake ni siku ya tarehe 2 Februari.
    Jaji Hanifa ameeleza kuwa ni vyema watanzania kutoka maeneo mbalimbali wakazitumia siku hizo ipasavyo kwa kutembelea banda lao kwani watapata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo mirathi, kukata rufaa, migogoro ya ardhi, haki za watoto kwa serikali, jamii na wazazi.
    Pia Jaji Hanifa ametaja manyanyaso ya kijinsia kama changamoto kwani wanawake wengi wamekuwa hawatoi taarifa kwenye mamlaka husika, hivyo amewataka watoe taarifa hizo kwenye mamlaka husika ili waweze kusaidiwa.
    Katika hatua nyingine banda hilo la TAWJA lilipata bahati ya kutembelewa na Katibu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania Jaji Sahel ambaye pia ni hakimu wa Mahakama ya Biashara.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI