
Mkuu wa shule ya Sekondari Halisi, iliyopo Kata ya Majohe Jacob Mosha,
pamoja Afisa elimu kata ya Majohe Nancy Peter, wamesimamishwa kazi kwa
kosa la kuchangisha michango wanafunzi wa shule hiyo shilingi 2500 ya
kitambulisho, na Nembo ya shule shilingi 4000.
Akizungumza shuleni hapo, Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es Salaam, Hamis
Lisu, amesema Mwalimu huyo amesimamishwa ili kupisha uchunguzi.
Lissu , akiwa ameambatana na Afisa Elimu Wilaya Elizabeth Ngonyani, na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Palela Msogela, baada ya kuzungumza na
walimu na wanafunzi shuleni hapo wamesema wanapata vitisho kutoka
kwa Mkuu huyo kuwa atakaye sema atafukuzwa ama kuhamishwa shule.
Amesema, kuchangia mchango wanafunzi ni kinyume cha Sheria waraka namba 3 wa elimu bila malipo wa mwaka 2016.
"Pamoja na kuwepo waraka huu nimekuta nimewasisitiza walimu
kutowachangisha wanafunzi kama vile haitoshi juzi tena baada ya Mh.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe kulizunguza na
kulitilia mkazo nimetuma Barua kwa Wakurugenzi kuwataka wote walikuwa
wamepewa vibali vya kuchangisha waache mara moja kwakuwa mkuu wa mkoa
alivifuta vyote". Amesema Afisa Elimu.
Pamoja na hayo amesema ataunda Kamati ikiongozwa na yeye na Mkurugenzi,
itaanza kazi ya uchunguzi Juma tatu tarehe 29 January na Mkuu wa shule
na Afisa Elimu kata ili kupisha uchunguzi wa Kamati na pia
amemwaagiza Mkurugenzi kutafuta mtu wakukaimu nafasi ya Mratibu kata.
Pia amewataka walimu ambao wanatishiwa maisha na Mkuu wa shule kubakia shule hapo na atakaye tishiwa atoe taarifa kwake.
Hata hivyo Mwalimu huyo amejitetea kuwa amewarudishia fedha zao wanafunzi wote aliwachangisha, na wanafunzi nao wameuthibitishia kurudishiwa fedha zao.
No comments:
Post a Comment