• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday 24 June 2017

    TAZAMA PICHA NA HABARI ZA DC SOPHIA MJEMA ALIVYOMUWAKILISHA WAZIRI MKUU KATIKA FUTARI ILIYOANDALIWA NA TAASISI YA MARIDHIANO TANZANIA


    ,

    Mkuuwa Wilaya ya ilala Mhe. Sophia Mjema  amezitaka taasisi zote za kidini nchini kuwa na ushirikiano wa pamoja katika masuala ya kijamii na kiimani ili kuimarisha umoja na kudumisha amani na
     mshikamano wa kitaifa.

    Mh Mjema ameyasema hayo jijini Dar es Salaam  katika Futari ya pamoja  iliyandaliwa na Taasisi ya ya Maridhiano Tanzania amabayo illiandaliwa kwa lengo la kuwaleta pamoja madhehebu ya Dini mbalimbali kutathinini mstakabali wa amani ya nchi .

    Aidha Mhe. Mjema amaesema taasisis za kidini nchini zina mchango mkubwa katika kudumisha amani ya nchi kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanawasikiliza viongozi wao wa kiro hivyo umoja wa viongozi hao utasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda amani

    Kwamujibu wa waandaaji wa Futari hiyo iliyodhaminiwa na Kampuni ya Super Doll ,watu wapatao  zaidi ya 400 walishisriki ,  ambapo wamesema utaratibu huu wa kufuturisha utakuwa endelevu na mwakani wamekusudia kufuturisha watu wapatao 1000.



    Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema  aliye upande wa kulia akiwa katika mazungumzo na moja ya wageni waalikwa katika futari iliyoandaliwa  na taasisi ya Mridhiano.Tanzania. 

     Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe. Sophia Mjema  akisalimiana na baadhi ya viongozi na wageni waalikwa  walio hudhuria futari katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.






     Katibu  mkuu wa Taasisi ya Maridhiano tanzania  Osward Mlay aliyeko katikati  akisalimiana na viongozi   mbalimbali wa   taasisis hiyo 








      Katibu  mkuu wa Taasisi ya Maridhiano tanzania  Osward Mlay aliyeko  akisisistiza jambo  wengine  ni moja wa viongozi   wa   taasisis hiyo













    Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe. Sophia Mjema  akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wageni waalikwa  katika futari ya taasisi ya Maridhiano Tanzainia

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI