• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 23 June 2017

    WAHAMIAJI HARAMU 45 WAKAMATWA WILAYANI MKINGA.

    IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga imewakamata wahamiaji haramu 45 kutoka nchini Ethiopia katika Kijiji cha Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa shambani kwa wananchi wanakula mahindi kabla ya kutiwa nguvuni.

    Licha ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao lakini pia idara hiyo inamshikilia raia mmoja kutoka
    nchini Kenya ambaye ndio alikuwa akiwaongoza wahamiaji haramu hapa.


    Akizungumza na waandishi wa habari,Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Crispin Ngonyani alisema wahamiaji
    haramu hao walikamatwa June 18 mwaka huu katika kijiji hicho baada kupata taarifa kutoka
    kwa wasamaria wema  wa eneo hilo.


    Alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa porini katika jiji hicho wakati wakisafiri kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo waligunduliwa na wananchi baada ya kufika mashambani mwao wakawakuta wanakula mahindi ndio walipotoa taarifa kwa askari wa Polisi wa Horohoro na hivyo wakaenda kuwakamata.


    Aliwataja wahamiaji haramu hao kuwa ni Melesa Manesha, Asaf Erisid,Ashnif Agide,Mulugeta Menano,Demek Sorebeto,Samal Latbo,Temesgen Tefera,Tememi Juheri,Mubarc Lamago,Temesa Kibemo,Haftamu Tumiso,Teshum Assfe,Yohanness Ayano na Daniel Abbate.


    Aidha Ofisa Uhamiaji huyo aliwataka wengine walio kamatwa kuwa ni Kibmam Abab,Temesgzeen Ayele,Akilu
    Abraham,Pxirose Makore,Munyasha Lombaso,Berekei Cezenzeni ,Detebo Erikato, Ayele Kebamo,Tamrat
    Mamo.


    Wengine waliokamatwa kuwa ni Saniel Wolde,Tomiot Deto Gem,Abeje Alemeyo, Ashenaf Waje,Tariko
    Dutamo,Birhanu Atso,Tesefaye Dena,Tekel Abush,Tesyfe Landu na Abdi Hassani.


    Kwa mujibu wa ofisa uhamiaji huyo aliwataja wengine kuwa ni Daafa Daimo,Getahun Zeleke,Yonas Liliso,
    Amanei Ashebo, Xesabo Womago,Isagay Tikie Mubarik Analo,Begaye Ganorem,Dawit Teso,Teshele
    Kemiso,Samweli Hyle na Tamasgen Sorsa.


    Alisema wahamiaji haramu hao wamefikishwa mahakamani jana kujibu tuhuma zinazowakabili akiwemo
    msindikizaji  Mongela Kidhome ambaye ni Mkenya na mkazi wa mpakani mwa Kenya na Tanzania
    Horohoro.


    Hata hivyo aliwataka mawakala wa wahamiaji haramu kuacha mara moja vitendo vya kuwaingiza
    nchini kwani watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma zinazowakabili.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI