Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
(kulia) akizungumza wakati wa mkutano na Ujumbe wa Mawaziri kutoka
Uganda. Katikati ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter na Waziri wa
Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
(kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na Ujumbe wa Mawaziri kutoka
Uganda (hawapo pichani). Katikati ni Kamishna wa Madini, Mhandisi
Benjamin Mchwampaka na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim Mruma.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
(mbele katikati) akizungumza wakati wa mkutano na Ujumbe wa Mawaziri
kutoka Uganda (kushoto) na baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi
zilizochini ya Wizara ya Madini (kulia).
Mawaziri kutoka Uganda wakimsikiliza
Waziri wa Madini nchini, Angellah Kairuki (hayupo pichani). Kutoka
kulia ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter, Waziri wa Nchi- Mambo ya
Ndani, Obiga Kania, Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala,
Namugwanya Bugembe na Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi, Dkt. Kasirivu
Atwooki.
Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka akiwasilisha mada ya masuala mbalimbali ya Sekta ya Madini, nchini Tanzania.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
(kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani wa Uganda, Obiga
Kania (kushoto). Katikati ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
amekutana na Mawaziri Wanne kutoka nchini Uganda ambao wamewasili nchini
Tanzania kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kubadilishana uzoefu
katika usimamizi wa Sekta ya Madini.
Mawaziri hao ni Waziri wa Nchi-
Madini, Lokeris Peter, Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania,
Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala, Namugwanya Bugembe na
Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi, Dkt. Kasirivu Atwooki.
Waziri Kairuki amekutana na ujumbe
huo Novemba 28, 2017 katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es
Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za
Madini nchini ikiwemo suala la Sera, Sheria na Kanuni za Madini pamoja
na masuala yanayohusu Wachimbaji Wadogo wa madini.
Majadiliano baina ya Wizara na Ujumbe
huo vilevile yalihusisha uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa
Kamishna wa Madini, Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO).
Ujumbe huo utatembelea migodi
mbalimbali ya Dhahabu inayomilikiwa na wazawa iliyoko mkoani Geita ili
kujionea uendeshaji wa migodi hiyo na hivyo kupata uzoefu wa namna ya
uendeshaji wake.
Aidha, ujumbe huo wa Mawaziri kutoka
nchini Uganda, utatembelea nchi mbalimbali Barani Afrika ili kupata
uzoefu wa usimamizi wa Sekta ya Madini hususan suala la Wachimbaji Wadogo.
No comments:
Post a Comment