Na Zuena Msuya, Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewateua Wahandisi Saba(7)
kutoka Wizara ya Nishati watakaoshirikiana na wakandarasi wanaotekeleza
Mradi wa REA III katika kila Kanda ili kuboresha na kurahisisha
utekelezaji wa Mradi huo kwa ufanisi.
Dkt. Kalemani alifanya uteuzi huo baada ya kufanya mkutano na
Wadau mbalimbali wanaotekeleza Mradi wa REA III wakiwemo, Wakandarasi,
Wawekezaji wenye Viwanda vya kutengeneza miundombinu ya umeme kama vile
Trasfoma, Mita, pamoja na nyaya za umeme , Mameneja wa Kanda, na
Wahandisi wanaosimamia Mradi ya REA III nchi nzima.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina ulipo
Makao Makuu ya Nchi Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine ulilenga
kujadili hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Umeme
Vijijini Awamu ya Tatu pamoja na changamoto zinazojitokeza katika
utekelezaji wa Mradi huo.
Dkt.Kalenani alisema Wahandisi walioteuliwa watashirikiana na
Wakandarasi wa REA III kutafanya kazi mbalimbali pamoja na kuwa na
mpango kazi wa kila wiki wa kila Mkandarasi katika eneo husika ili
kusisimamia kwa ukaribu utekelezaji wake.
Pia watarahisisha mawasiliano yamoja kwa moja kutoka kwa
wakandarasi hao na Wizara ya Nishati ili kufahamu hatua waliofikia na
changamoto watakazokuwa wakikabiliana nazo kwa Lengo la kuzitafutia
ufumbuzi wa haraka.
No comments:
Post a Comment