Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye baada ya kusikia sauti ya Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu ambaye tangu alipopigwa
risasi haijawahi kusikika sauti yake amemuomba mbunge huyo atulie mpaka
apone kabisa.
Nape amesema anamuombea Mbunge apone kwanza huku akisema anamshukuru Mungu kwa kuliona tabasamu lake.
Mjomba tunamshukuru Mungu kwa tabasamu hili la
matumaini!Nakuombea afya iimarike kabla hujasema mengi!Tulia mjomba
upone kabisa kwanza! ameandika Nape kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo, hivi karibuni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe
alisema kuwa hali ya mbunge huyo imeimarika zaidi na vifaa vilivyokuwa
vikiusapoti mwili wake vimeondolewa na sasa mwili wake unajiendesha
wenyewe.
Mh. Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu
eneo la ‘area D’ mjini Dodoma na watu wasiojulikana. Ambapo kwasasa
anapatiwa matibabu Nairobi Kenya.
..
Thursday 19 October 2017
Habari
Home
Breaking News
Habari
Maneno ya Mbunge Nape baada ya kusikia sauti ya Mh. Lissu ‘Tulia mjomba upone kabisa’
No comments:
Post a Comment