• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 30 January 2017

    Mrisho Mpoto alia na umoja wa wasanii

    Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewataka wasanii kuondoa makundi yaliyopo kwenye muziki na kuanza kushirikiana kwa pamoja ili kuleta mafanikio kwa wengi.
    Akiongea na mwandishi wetu Jumatatu hii muimbaji huyo amedai kila msanii nchini anafanya kazi kivyake hali ambayo inawanyima zaidi wasanii fursa za kibiashara.
    “Kwa muda mrefu sasa wasanii wa Tanzania wamekua wakifanya kazi nzuri ndani na nje ya nchi, lakini kila mtu anacheza karata yake kivyake kutokana na network na nguvu yake,” alisema Mpoto. “Nadhani sasa wakati umefika kuondoa tofauti zetu, makundi, tukawa team moja tukae tuone tunawezaje kusaidiana kwenye nyanja za kibiashara,”
    Aliongeza, “Kuwa kama wasanii wa Taifa la Tanzania wenye muelekeo mmoja bila kuingilia fani ya mtu wala maisha binafsi, Wazo langu tusitawanyike ikawa kila mtu anaenda kivyake, ukiotea hit basi ndiyo unapata hela, najaribu tu kuwaza kwa sauti kama wazo lina mashiko, #teamtanzania,”
    Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao wanapiga deal nyingi nje ya muziki ukiachia mbali deal za ubalozi za makumpuni mbalimbali alizopewa

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI