• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday 29 January 2017

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya ufunguzi wa jengo la Upasuaji kwa wanawake wajawazito

    kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya ufunguzi wa jengo la Upasuaji kwa wanawake wajawazito
     katika Hospitali ya Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni jengo lilidhaminiwa na Taasi ya GSM Foundation, ambapo jengo
     hilo limepewa jina la Makonda Obstetric Theatre kutokana na yeye kuwa muasisi wa jitihada hizo za ujenzi alipokuwa
     Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli March 13 Mwaka jana kuwa Mkuu wa Mkoa
    Akizungumzia ujenzi wa jengo hilo RC Makonda amewapongeza GSM Foundation na kuwataka watanzania waunge mkono

     jitihada za wawekezaji wanao wekeza ndani ya nchi na kuwataka wananchi kununua bidhaa za wazawa kwani mwisho wa siku wanairejesha
    faida kwa wananchi kwa kufanya miradi ya maendeleo kama hiyo, huku akisisitiza suala la ulipaji kodi kwa kila mtanzania serikali yeyote duniani haiwezi
     kujiendesha bila ya kulipa kodi ndiyo maana Rais Magufuli anasisitiza kulipa kodi, hivyo kila mtanzania ajue anamchango katika maendeleo ya taifa kwa kulipa kodi .

    Akitoa Muhtasari waMradi Mhandisi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya GSM Foundation waliodhamini ujenzi huo Hersi Saidi
    ameeleza kuwa ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 420 na kuna vyumba viwili vya upasuaji,
     huku akisisitiza kuwa watanzania wawe na moyo wa kujitolea kama walivyofanya wao.

    Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta
     ameeleza kuwa jengo hilo ni muhimu sana kwani linauwezo wa kuhudumi kinamama kati ya 40 na 50 kwa siku hivyo
     kati ya wanawake 20 na 30 ufanyiwa upasuaji na kupelekea kuondoa msongamano uliokuwepo awali
    na kufanya huduma zichelewa, pia utaokoa maisha ya wanawake.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI