• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 30 January 2017

    DAS Mpogolo afungua Bonanza la Michezo na kutoa nasaha hizi



    Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka Vijana kuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara kwani kufanya hivyo kunapelekea Afya zao kuwa imara na kuepuka magonjwa yanayoweza sababisha vifo vya mapema.
    Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bonanza la Michezo maeneo ya Tabata lililoandaliwa na Windhoek beer DAS Mpogolo amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) vijana wengi wanapoteza maisha kwa kutotunza Afya zao na kueleza kuwa vifo takribani 3000 vimeripotiwa vinavyotokana na shinikizo la damu huku Tanzania ikiwa nchi ya 85, huku kwa ugonjwa wa kisukari watu takribani 9257 wamepoteza maisha na Tanzania ikishika nafasi ya 35 kidunia na Kiharusi zaidi ya 5000 wamepoteza maisha na Tanzania ikishika nafasi ya 102 kidunia.
    Kutokana na Takwimu hizo DAS Mpogolo amesisitiza mazoezi kwa vijana kwa kufanya michezo ambayo inawakutanisha na kuanzisha mahusiano na kuleta undugu, huku akiwasisitiza waandaaji waandae mabonanza kama hayo yakishirikisha michezo ya aina tofauti siyo mpira wa miguu pekee.
    Bonanza hilo lilikuwa kivutio baada ya Timu mbili za Kwetu Pazuri wakiwa wenyeji na Bongo Fleva, huku timu ya Kwetu Pazuri ikiwa na wachezaji ambao ni wasanii wa familia moja Ali Kiba na Abdul Kiba na mchekeshaji maarufu kama Kupe ambaye aliipatia ushindi Kwetu Pazuri kwa kushinda goli mbili kwa nunge, na kwa upande wa Bongo Fleva timu yao ilipambwa na mastaa wakongwe akiwemo KR, Mchizi Mox, Soggy Doggy, Suma G, M2THE P, na Juma Nature.
     



    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI