• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 30 January 2017

    HESLB: Mwajiri asiyetoa ushirikiano kufichua wadaiwa atachukuliwa hatua.

    Wakati Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu nchini ikiendelea na msako wake ofisi kwa ofisi ambapo ni wiki moja baada ya kutimiza awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya ukusanyanji wa madeni ya wadaiwa sugu kupitia kwa wajiri wa makampuni mbali mbali jijini Dar es Salaam Bodi imeomba ushirikiano kutoka kwa waajiri.
    Mkurugenzi msaidizi wa urejeshaji wa mikopo Phidelis Joseph amewataka waajiri wanapo ajiri wafanyakazi wanatakiwa kupeleka ripoti ya waajiriwa kwenye bodi ya Mikopo ya Wanafunzi kwa ajili ya kuhahakiki majina ili kurahisisha kuwajua wanafunzi wanao daiwa na endapo watalipuuzia swala hilo watapewa faini ya asilimia 10% ya deni la mdaiwa.
    “Tutahakikisha kuanzia sasa kila mwajiriwa anakatwa 15% pia endapo watachelewesha tutawafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria” alisema Philides.
    Aidha Joseph amewataka walio jiajiri kurejesha madeni hayo kwa mwezi laki moja, pia wajiriwa na wajiri walio mikoani nao wanatakiwa kuhakikisha wanalipa madeni hayo kabla kamati ya kampeni kufika mikoani kwani endapo watalipuzia itapelekea kutozwa faini

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI