Uongozi wa klabu ya Simba chini ya Rais
‘Try again’ umemtambulisha rasmi kocha wao mpya Pierre Lechantre raia wa
Ufansa pamoja na kocha wa viungo Mohammed Aymen Habibi ambaye ni raia
wa Morocco.
Makocha hao Pierre Lechantre (kocha mkuu) na Mohammed Aymen Habibi (kocha wa viungo) wamesaini mikataba na klabu ya Simba lakini mikataba hiyo haijawekwa wazi ni ya muda gani wala thamani ya mikataba hiyo kutokana na makubaliano ya pande mbili (Simba kama timu na makocha hao).
Baada ya kusaini mkataba kisha kutambulishwa mbele ya wanahabari kocha mkuu wa Simba amesema ili kuzishinda klabu nyingine kubwa za Afrika ni lazima uwe na kikosi bora na ndio maana amekuja Simba.
“Nimeiona jana Simba ikicheza, nimefurahi kuiona ikishinda magoli manne, nitashirikiana vizuri na kocha msaidizi (Masoud Djuma) ili kufanya vizuri zaidi.
“Nipo hapa kwa ajili ya kufanya kazi, masuala ya CV tuweke pembeni kwanza.
“Ili kupata mafanikio Afrika ni lazima uwe bora na ndio maana nipo hapa.
Kocha huyo ataanza kazi rasmi mara timu itakaporejea kutoka Kagera ambako imekwenda kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar.

No comments:
Post a Comment