Kesi inayowakabili wafanyabiashara maarufu ya kuhujumu uchumi na kuitia
serikali hasara ya mamilioni ya pesa, imezidi kugubikwa na utata dhidi
ya afya za watuhumiwa wake, James Rugemarila na Habinder Sethi.

Taaifa hiyo ilipingwa na wakili wa Rugemarila, Respicious Didas, ambapo alieleza kuwa suala la ugonjwa wa mteja wake upo wazi kwamba ana uvimbe unaoonekana.
“"Licha ya ugonjwa wa mteja wangu kuwa wazi, bado upande wa mashtaka haujachukua hatua yoyote kuhusiana na uvimbe huo, linapaswa kupewa kipaumbele na ugunduzi wa ugonjwa wake ufanyike kwa kutumia madaktari wa India”, amesema Wakili Didas.
Pamoja na hayo Wakili huyo ameendelea kuelezea kuwa mteja wake aliwahi kuugua saratani na kufanyiwa upasuaji mwaka 2008, na kwamba ugunduzi huo pamoja na matibabu yote, vilifanyika nchini India, baada ya vipimo vilivyokuwa vinafanyika hapa nchini vilikuwa vina shida, na ndio sababu aliamua kuanzisha kituo cha saratani hapa kwa ajili kusaidia wananchi wasio na uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya nchi, waweze kupata matibabu katika kituo chake.
kwa upande wa mshtakiwa mwengine ametakiwa kufanyiwa upasuaji wa kutoa puto lililpo tumboni mwake linalodaiwa kuwa limeisha muda wake, kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, chini huku madaktari wake waliokuwa wakimtibia awali kutoka nchini Afrika Kusini wakiwepo pia.
Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo ameutaka upande wa mashtaka kusimamia matibabu ya watuhumiwa hao Rugemarila pamoja na Seth, na kuahirisha kesi hiyo mpaka Februari 2, 2018
No comments:
Post a Comment