
Kwenye ripoti iliyotelewa leo, HRW ilisema kuwa kuna maelfu ya wafanyakazi wa nyumbani kutoka Tanzania wako nchini Oman na UAE.
Watafiti wake waliwahoji 50 kati yao na kugundua kuwa karibu wote walipokonywa pasipoti zao walipowasili na kulazimiswa kufanya kazi hadi masaa 21 kwa siku bila kupumzika.
Wafanyakazi waliotoroka waajiri dhalimu na maajenti walisema kuwa polisi au balozi zao ziliwalazimisha kurudi la sivyo wangekosa mishahara yao hali iliyowachukua muda mrefu kutafuta pesa za kuwawezesha kurudi nyumbani.
Walisema kuwa walilipwa pesa kidogo kuliko zile waliahidiwa, au walikosa kulipwa kabisa, wakalazimishwa kula chakula kulichooza au mabaki ya chakula na kutukanwa kila siku, na pia kudhulumiwa kingono
No comments:
Post a Comment