Na.
MWANDISHI WETU
Ofisi
ya Waziri Mkuu imeendesha warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Sheria Ndogo inayohusu Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa maafa kwa
lengo la kuwajengea uwezo wa masuala ya Menejimenti ya maafa nchini.
Akizungumza
wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Novemba 12, 2017 Makamu Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mhe.William Ngeleja alieleza kuwa warsha hiyo itawajengea uwezo wajumbe wa
Kamati hususani katika utekelezaji wa majukumu yao.
"Warsha
hii ni muhimu kwa wajumbe wa kamati kwani itaongeza uelewa kuhusu sheria ya
Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 pamoja na dhana nzima ya Menejimenti
ya Maafa"
Akifanua
mhe.Ngeleja amesema warsha hiyo itasaidia kuongeza tija katika utendaji wa
kamati hasa katika kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya maafa.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama aliwaeleza wajumbe kuwa Serikali inaendelea
kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini ili
kujenga uwezo wa Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali pindi maafa
yanapotokea hivyo warsha hii inatija kwa wajumbe wote.
"Warsha
hii itasaidia kuongeza uelewa kwa wajumbe kuhusu namna bora ya kupambana na
majanga yanapoytokea nchini na madhara yake, vyanzo na sababu za kutokea, hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia, kupunguza madhara, kujiandaaa , kukabili na kurejesha
hali katika ubora zaidi" Alisisitiza Mhe. Mhagama.
Sambamba
na hilo Mhe. Mhagama alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua
mbalimbali ikiwemo kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini kwa
kuanzisha Idara ya uratibu wa maafa inayotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa
sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Pamoja
na hatua hizo Serikali ina sera ya Taifa ya Usimamizi wa maafa ya mwaka 2004 ambayo
inaeleza hatua na majukumu ya wadau mbalimbali katika shughuli za Manejimenti
ya maafa na kutoa muongozo wa utekelezaji wake.
Aidha
mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Mhe.Elibariki Kingu alipongeza Ofisi ya Waziri
Mkuu kwa kuendesha warsha hiyo na kushauri serikali kuwekeza zaidi katika
kupambana na majanga yanayoweza kujitokeza hapo nchini.
AWALI
Mada
zilizowasilishwa katika warsha hiyo zilijikita katika Dhana, Sheria na Mfumo wa
Usimamizi wa Maafa hapa nchini ikiwa ni moja ya jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu
kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuwajengea uwezo wadau na wananchi kwa
ujumla ili kuweza kuyakabili maafa pindi yanapotokea. Warsha ilikuwa ya siku
moja iliyojumuisha wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo
kuhusu masuala ya Menejimenti ya Maafa iliyofanyika Bungeni Dodoma
No comments:
Post a Comment