Katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara katika eneo la
Ubungo mjini Dar es salaam,Rais Magufuli ameagiza sehemu ya jengo ambalo
ni makao makuu ya shirika linalozalisha na kusambaza umeme, TANESCO,
kuwekwa alama ya 'X' kuashiria jengo hilo libomelewe.
Jengo jingine ambalo litaathiriwa na agizo hilo ni jengo la wizara ya maji ambalo lipo jirani.
Imeagizwa majengo hayo kubomolewa kutokana na kuwa yamejengwa katika sehemu ya hifadhi ya barabara.
Zoezi
la bomoa boma limekuwa likiendelea, ambapo majengo pembezoni ya
barabara inayounganisha mji wa Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi
yameathirika. Wakaazi wengi waliokuwa wakiishi katika maeneo yanayodaiwa
kuwa katika hifadhi ya barabara wamepoteza makazi yao.
..

No comments:
Post a Comment