• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 13 November 2017

    Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika onesho La picha ili kujionea kazi na fursa mbali mbali kutokana na maisha ya watanzania miaka 50 iliyopita.




    Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa makumbusho ya Taifa Bw.Audax Mabula alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na onesho hilo ambapo amesema onesho hilo limeandaliwa na  makumbusho ya taifa kushirikiana na mpiga picha Bw.jesper Kirknaes na kudhaminiwa na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania hivyo onesho hilo litafunguliwa rasmi na Mh.Balozi Einar .H.Jensen kutoka ubalozi wa Denmark nchini Tanzania tarehe 16 mwezi huu saa 7 mchana eneo la makumbusho hivyo viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.


    Hata hivyo Bw.Mabula amesema katika onesho hilo linaitwa "Karibu Tanzania" ambapo ameeleza kuwa picha mbalimbali zinazohusu maisha na kazi zilizokuwa zilizokuwa zinafanywa na watu wa enzi hizo zitatoa mwanga na ufumbuzi wa kifikra kwa kila mmoja kwani zinaonyesha na kueleza maisha halisi ya watanzania hao waliokuwa mwaka 1968-1977 namna walivyoweza kutengeneza vifaa mbali mbali kama vyungu,majembe na kila kitu ambacho walichokuwa wanahitaji kwa wakati huo.


    Vile vile Bw.Mabula amewataka zaidi vijana kujitokeza katika onesho hilo kwani watajifunza tamaduni mbalimbali za makabila yao kwa kuona nyumba halisi za makabila yao,vyombo vyao vya nyumbani kama chungu,vikapu na kadhalika hivo onesho hilo linaumuhimu zaidi .


    Pia Mabula ameongeza kwa kusema kwa wakati huu tuliopo wa Sera za viwanda tunapata funzo kutoka kwa watanzania wenzete ambao waliweza kuendesha maisha yao kwa kujitengenezea wenyewe vitu walivyovihitaji wenyewe hivyo kupitia picha hizo tunaweza kuona tulipotoka na kujifunza fursa zaidi kwani tunaweza kuviendeleza baadhi ya viwanda vilivyoachwa na watu hao kwa kujifunza kutengeneza wenyewe baadhi ya vitu kama majembe na vingine vingi kwani kupitia picha hizo zinaonyesha hatua kwa hatua walizokuwa wanazifanya watanzania wenzetu.


    Naye mpiga picha hizo Bw.Jensen Kirknaes amewataka watanzania waje kwa wingi katika onesho hilo kwani kila picha moja inamaana chanya zaidi ya elfu moja  hivyo anaamini watanzania watajifunza Vingi kupitia onesho hilo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI