• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 29 January 2018

    Ofisi ya takwimu taifa yatoa elimu kwa wananchi

    Ofisi ya takwimu ya taifa imesema kuwa inajukumu la kuhakikisha takwimu zinazozalishwa katika vyanzo vya takwimu zinakidhi kanuni stahiki ili kuondoa kukinzana kwa takwimu wakati wa kufuatilia Mipango ya maendeleo ya wananchi.

    Hayo amesema leo mkurugenzi mkuu wa takwimu taifa Dkt. ALBINA CHUWA wakati wa semina ya uelimushaji umma kuhusu sheria ya takwimu ya mwaka 2015 ambayo inawapa fursa wananchi kuelewa Kwa kina dhana ya takwimu rasmi na tofauti iliyopo kati ya takwimu rasmi na takwimu nyingine.

    Aidha Dokt. Chuwa amesema kuwa Serikali kupitia ofisi ya takwimu nchini inawaasa jamii kutokukubali kupokea takwimu ambazo hazija thibitishwa na taasisi zilizopewa kibali ya kutoa takwimu nchini.
       
    Kwa upande wa wadau hao wameiomba kushirikiana  kwa pamoja na taasisi ya takwimu Taifa wakati wakutoa takwimu ili kujilidhisha  data zinazotolewa kwa wananchi.

    Ameongeza kuwa ili takwimu ziwe rasmi nilazima ziwe zinafuata sheria ya takwimu kwani ni kosa la jinai Kutoa takwimu isiyo rasmi kwa mujibu wa sheria ya takwimu nchini.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI