• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 23 August 2016

    Aga Khan kuokoa hadi bil 25/- za matibabu nje



    SERIKALI imezindua ujenzi wa jengo la Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam ambao ukikamilika, utawezesha kutolewa kwa matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza yakiwamo ya saratani, moyo na figo na hivyo kusaidia kuokoa Sh bilioni 20 hadi 25 zinazotumika kila mwaka kwa ajili ya rufaa za wagonjwa wanaotakiwa kutibiwa nje ya nchi.
    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizindua kuanzishwa kwa awamu ya pili ya ujenzi wa jengo hilo likitarajiwa kuwa na vitanda 170 utakapokamilika.
    Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Kamati ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taasisi ya Afya ya Aga Khan, binti wa Mfalme Aga Khan, Princess Zahra Aga Khan.
    Alisema serikali imejikita kujenga uwezo wa ndani ili matibabu ya magonjwa mbalimbali yatolewe nchini kwa kushirikiana na wabia mbalimbali.
    Naye Princess Zahra alisema taasisi hiyo ya afya sio kwa ajili ya kutengeneza faida, bali inalenga kutoa huduma bora, imara kwa Watanzania.
    Alisema hospitali hiyo imetoa ajira kwa watu 1,000, ikihudumia wagonjwa wa nje zaidi ya 430,000 wa ndani 7,000 pamoja na kutoa huduma mbalimbali za vipimo

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI