SERIKALI imeliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu wakati wa kukabiliana wahalifu wanaofanya mauaji na kuvuruga amani ya nchi, huku ikiwahimiza wananchi kutii sheria kwa kujiepusha kushiriki katika vitendo viovu kwenye jamii.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na askari wa vikosi mbalimbali vilivyopo chini ya wizara hiyo wakati wa ziara yake mkoani Tanga.
Alisema katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya makundi ambayo yanashawishi wananchi ili washirikiane nao kuvunja sheria huku mengine yakishabikia vitendo vya mauaji na uhalifu wa aina mbalimbali unaofanywa nchini kwa lengo la kuvuruga amani.
Akizungumzia uwepo wa biashara za magendo, ametaka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kufichua uingizwaji wa bidhaa mbalimbali za magendo, wahamiaji haramu na kukomesha uuzaji wa dawa za kulevya kwa kutoa taarifa.
Awali, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Godwin Gondwe akisoma taarifa ya mkoa, alisema hali ya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo imeimarishwa ikiwemo katika Mapango ya Majimoto yaliyoko Amboni ambako kulivamiwa na wahalifu limedhibitiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakuliyamba alisema katika kipindi cha Juni mwaka huu vitendo vya uhalifu unaosababisha mauaji vimepungua mkoani humo ikilingashwa na kipindi kilichopita
No comments:
Post a Comment