• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 18 August 2016

    ANC chaanguka katika uchaguzi Pretoria

    Bendera ya African National Congress (ANC) cha nchini Afrika KusiniCHAMA cha African National Congress (ANC) ambacho kinatawala nchini Afrika Kusini  cha kimepoteza udhibiti baada ya kushidwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Pretoria, anaandika Pendo Omary.
    ANC kimeshindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika eneo hilo, baada ya kuzidiwa nguvu na chama cha Democratic Alliance ambapo matokeo yanaonesha kuwa chama cha Democratic Alliance kikipata 43 asilimia  ya kura na ANC 41 asilimia.
    Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripoti kwamba chama cha Democratic Alliance kitalazimika kuunda serikali ya mseto kuongeza udhibiti katika eneo hilo, ambapo pia ANC na Democratic Alliance vinachuana vikali kudhibiti mji wa Johannesburg, ambao ni mji mkubwa kabisa nchini humo.
    Katika uchaguzi huo ANC kikiwa moja kati ya vyama vikogwe vilivyo madarakani barani afrika kimepata matokeo mabaya zaidi tangu kuanzishwa kwake.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI