• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 27 August 2016

    Chombo cha anga za mbali cha NASA chamudu kuichunguza sayari ya Jupita


    Chombo cha Juno kikizunguka sayari ya jupitaImage copyrightNASA
    Image captionChombo cha NASA -Juno kitasafiri mara 30 kuzunguka sayari ya Jupita wakati wa safari yake itakayomalizika mwaka 2018
    Shirika la safari za anga za mbali la Marekani NASA limetuma chombo chake kilometa elfu kadhaa kutoka kwenye mawingu madogo juu ya sayari ya Jupita, sayari kubwa zaidi katika mfumo wa jua.
    Hakuna Setilaiti nyingine iliyowahi kusafiri karibu sana na Jupita katika awamu kuu ya safari yake.
    Chombo hicho cha anga za mbali- Juno spacecraft- kilisafiri kilomita 200,000 kwa saa kilipopitia tu , kwa matumaini ya kuchukua picha na taarifa kuhusu sayari hiyo na mfumo wake wa hali ya hewa.
    Shirika la NASA linachunguza sayari hiyo imeundwa na nini, na muundo wake kwa ujumla.
    Chombo hicho kiliingia kwenye uzio wa Jupita tarehe 5 Julai baada ya kusafiri kwa miaka mitanno, safari ya kilomita bilioni 2.8 kutoka duniani.
    Chombo hicho kinatarajia kupita tena kwenye sayari ya Jupita mara thelathini na tano kabla ya safari yake kumalizika mnamo mwaka 2018.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI