UONGOZI wa Serikali katika Kata ya Ihumwa, Manispaa ya Dodoma umeeleza wasiwasi wa kuibuka migogoro ya ardhi eneo lao, ikiwemo ya kuuza eneo moja kwa zaidi ya mtu mmoja kutokana na uuzaji wa kimya kimya baada ya serikali kuzuia watu binafsi kufanya mauziano.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi katika ofisi ya Mtaa wa Chang’ombe katika Kata ya Ihumwa, Mwenyekiti na Mtendaji wa mtaa huo, walisema katika siku za hivi karibuni, kumekuwapo na wimbi la watu kutoka maeneo mbalimbali, ambao wamekuwa wakitafuta viwanja baada ya kusikia kuwa litakuwa maalumu kwa ofisi za serikali.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Chang’ombe, Samwel Masakauta na Mtendaji wa mtaa huo, Lister Sakalani, walisema licha ya kwamba wamezuiwa kuuza maeneo na kuambiwa yako chini ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), lakini imebainika wapo baadhi ya wenyeji wanaodaiwa kuendelea kuuza maeneo bila kuhusisha ofisi za mtaa.
“Huko nyuma, kabla ya tamko, walikuwa wakifika maeneo ya watu wa kawaida, wakazungumza na kisha kuja kutushirikisha. Lakini sasa tumepewa maelekezo kwamba tusiendelee kuuza maeneoa ...lakini wapo wanaouza kimya kimya suala linaloweza kuzua migogoro,” alisema Masakauta.
Naye Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Ihumwa, Sakalani, alisisitiza kuwa Mkuu wa Mkoa alishatoa tamko kwamba maeneo yasiuzwe.
“Wanakijiji tumewaambia juu ya hilo tamko. Hata Mbunge alikuwepo hivi karibuni na tukatangaza kuwa watu wasiuze maeneo,” alisema Sakalani.
Wakielezea hofu ya kuibuka madalali, viongozi hao walisema wapo watu ambao wamekuwa wakienda kimya kimya kwa wenyeji na kuingia makubaliano ya kuuziana na baada ya kujikuta wakiuziwa watu wawili eneo moja, ndipo hushirikisha uongozi wa mtaa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana ofisini kwake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Melkion Komba alisema wanaendelea kutumia watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha watu hawauzi maeneo
No comments:
Post a Comment