• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 20 August 2016

    Kamati ya Bunge yammwagia sifa DED Msalala



    KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imemmwagia sifa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, Simon Berege kutokana na kufanya mapinduzi makubwa katika kipindi kifupi tangu ateuliwe na Rais Dk John Magufuli kushika wadhifa huo.
    Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vedustus Ngombale akimmwagia sifa Berege, alisema ana imani kuwa ataifikisha mbali halmashauri hiyo kutokana na utendaji wake na kama kamati ya bunge lazima wampongeze kwa hilo.
    “Halmashauri ni changa ila kuna urasimu mkubwa uwe makini katika utendaji kazi wako, kuwa makini na wakuu wako wa Idara usipokuwa makini mwisho wa siku yatakuangukia wewe,” alisema Ngombale.
    Pamoja na Ngombale kutoa sifa hizo, mjumbe mwingine, Amina Makilagi akisema Mkurugenzi huyo atafika mbali.
    “Nenda kasimamie maagizo yote ya kamati umeanza vizuri ukasimamie vizuri halmashauri na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuwapatia ufumbuzi, nazungumza kama mzazi, kama mama kwa utendaji mzuri ulioanza utafika mbali,” alisema Makilagi.
    Mkurugenzi huyo alipewa pongezi, ikiwa ni siku moja Kamati hiyo iliposhindwa kupata majibu ya kujitosheleza kutoka kwa halmashauri ya Nachingwea ambayo Mkurugenzi wake Bakari Mohamed Bakari aliieleza kuwa ni mgeni hivyo majibu mengi yalitolewa na wataalamu wengine.
    Katika mahojiano ya juzi, Berege alionesha kujiamini zaidi katika kujibu maswali ya wilaya yake huku akija na pendekezo la kudai Sh bilioni 4.9 kutoka mgodi wa Acacia ambazo zimekuwa zikidaiwa bila ya mafanikio.
    Berege alitaka serikali kusaidia upatikanaji wa fedha hizo kwani zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo wilayani kwake huku akiahidi kuondoa mapungufu yaliyokuwepo katika taarifa za 2013/14.
    Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mibako Mabubu alisema madai ya fedha hizo yamekuwa yakizuiwa na baadhi ya wakubwa serikali bila ya kujua ni kwa sababu gani.
    Mabubu alisema waliitwa halmashauri tatu ambako kampuni hiyo ina migodi yake, hata hivyo walipodai fedha hizo walikatishwa tamaa baada ya viongozi kuwakemea hadi Mkuu wake wa wilaya Benson Mpesya akapata shinikizo la damu na kulazwa.
    Ngombale alimtahadharisha Mkurugenzi huyo kutokulewa sifa na badala yake atambue kuwa ziko changamoto nyingi kwenye halmashauri ikiwemo matatizo ya watumishi.
    Alimwagiza fedha za wanawake Sh milioni 348 na zile zilizochotwa zirudishwe na kwamba taarifa ya jinsi ya kuzirejesha ipelekwe LAAC kabla ya Septemba 10, mwaka huu pamoja na kumtaka kuimarisha kitengo cha uhasibu na kuacha kutumia fedha taslimu kinyume cha Sheria na Taratibu.
    Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela alisema maelekezo ya kamati yatafanyiwa kazi na watasimamia kazi zote vizuri ikiwemo kuimarisha utendaji

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI