Waendesha mashtaka nchini Afrika kusini wamekanusha taarifa za vyombo vya ndani vya habari kuhusu waziri wa fedha , Pravin Gordhan, kuwa anaweza kushtakiwa kwa ufisadi.
Mamlaka ya waendesha mashtaka nchini humo imesema kuwa polisi wamekabidhiwa taarifa zinazohusiana na tuhuma hizo kutoka kwa kile kinachojiita kitengo cha ujambazi kilichoanzishwa kwenye shirika la kodi.Hata hivyo jambo hilo lilihitaji kusomwa kwa ushahidi.
Bwana Gordhan amekataa kuulizwa jambo lolote na polisi kuhusiana na kitengo hicho cha ujambazi, ambacho kinadaiwa kuwapeleleza wanasiasa alipokuwa mkuu wa ofisi ya kodi.
Upinzani umeitisha mjadala wa kibunge wa kile wanachosema kuwa ni jaribio la wanaomuunga mkono rais Jacob Zuma la kumdhalilisha waziri wa fedha.
No comments:
Post a Comment