• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 22 August 2016

    Mapokezi makubwa yamsubiri Felix



    WANARIADHA wa Tanzania walioshiriki Michezo ya 31 ya Olimpiki wanatarajiwa kupata mapokezi makubwa watakaporejea nchini keshokutwa, licha ya kutopata medali.
    Mwanariadha Alphonce Felix alimaliza wa tano katika marathon kwa kutumia saa 2:11:15, huku wenzake wawili, Said Makula na Fabian Joseph wakimaliza katika nafasi ya 43 na 112 kwa muda wa saa 2:17:49 na 2:28:31.
    Mbali na kuandaliwa maandalizi ya aina yake, pia Felix amepongezwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo kwa kuvunja rekodi ya Juma Ikangaa aliyoweka mwaka 1988 katika Olimpiki ya Seoul, Korea Kusini akitumia saa 2:13:06. Ikangaa alimaliza mbio hizo katika nafasi ya saba.
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimpongeza mwanariadha huyo kwa hatua aliyofikia na kusema licha ya kutopata medali lakini nafasi ya tano ni kubwa.
    Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alimpongeza Felix na kusema kuwa, amejitahidi na kama wangeandaliwa kwa muda mrefu wangeweza kufanya maajabu.
    Alisema kuwa Felix kama akiandaliwa vizuri anaweza kupata medali katika Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo mwaka 2020. Kaimu Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla alimpongeza Felix na kusema kuwa sasa wako katika vikao vya kupanga jinsi ya kumpokea mwanariadha huyo na wenzake.
    Alisema wanafikiria wapi pa kufikia wanariadha hao, ambako pia wataandaliwa tafrija fupi, ambako watapewa zawadi, ambazo hata hivyo hakutaka kuzitaja.
    Alisema kampuni ya TTCL imefurahishwa na mafanikio ya Felix na wako tayari kufanya mazungumzo na RT ili kusaidia maandalizi ya wanariadha wa Tanzania katika mashindano mbalimbali.
    Alisema keshokutwa watakapowasili wanariadha hao watakaa na TTCL kuangalia jinsi ya kuusaidia mchezo huo ambao Tanzania ilivuma miaka ya nyuma.
    Felix alizaliwa Februari 14 mwaka 1992, muda wake bora binafsi ambao pia ndio uliomwezesha kufuzu kwa Olimpiki ni saa 2:09:19 aliouweka Otsu, Japan Machi 6, mwaka huu. Mwanaraidha wa kike, Sara Ramadhani alishiriki mbio za marathoni Jumapili ya wiki iliyopita na kumaliza katika nafsi ya 121 kwa kutumia saa 3:00:03

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI