IMEANDIKWA NA aziza DODOMA
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) imeiagiza Benki ya Posta (TPB) kufanyia kazi kasoro mbalimbali, ikiwemo zinazohusu utaratibu wa kutoa mikopo; zilizobainika katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha wa 2015.
Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly alitoa maagizo hayo jana mjini hapa na kusema upungufu huo, ikiwemo unaohusu ulinzi na usalama wa benki na watumishi wake, utatuliwe kabla ya mwakani kamati itakapokutana na benki hiyo tena kama ilivyofanyika jana mjini hapa.
Maagizo hayo yalitolewa baada ya kamati kukutana na kupata maelezo kutoka kwa viongozi na watendaji wa benki hiyo juu ya masuala mbalimbali yaliyobainishwa katika ripoti ya mdhibiti.
Hata hivyo katika kikao hicho, Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru, aliisifia TPB na kuitaja kuwa ni mfano wa kuigwa kwa mashirika ya umma kutokana na inavyojiendesha kwa ufanisi kwa kutumia faida inayopata.
Akisoma maagizo ya kamati, Aeshi ambaye ni Mbunge wa Sumbawanga Mjini ameitaka benki kurekebisha utaratibu katika utoaji mikopo, ikiwa ni pamoja na kufanya jitihada za kupunguza mikopo isiyolipika kuepuka kuingia hasara.
Maagizo mengine kwa benki hiyo ni kukamilisha udhibiti wa kiusalama kutokana na CAG kubainisha kasoro katika ulinzi na usalama wa benki na watumishi wake. Pia imeagizwa ikamilishe mchakato hatimaye ijiendeshe kama kampuni.
Awali, watendaji wa benki hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Lettice Rutashobya, wakijieleza kuhusu kasoro katika utoaji mkopo, ikiwemo mwombaji kuongezwa kiasi tofauti na alichoomba, ilielezwa kuwa tatizo ni ukosefu wa mfumo wa kisasa.
Katika kuelezea mikakati ya benki ikiwemo kujiendesha kwa mfumo wa kampuni, Mkurugenzi wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema mchakato wa kujiunga na soko la hisa umeanza
No comments:
Post a Comment