UKOSEFU wa huduma ya maji safi na salama katika Tarafa ya Bukene wilayani Nzega mkoani Tabora, umesababisha kituo cha afya cha tarafa hiyo kushindwa kufanya upasuaji na kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaolazimika kufuata huduma hiyo katika hospitali ya wilaya ya Nzega iliyopo umbali wa Kilometa 40.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wa tarafa hiyo walisema wamekuwa wakitumia maji ya madimbwi na visima ambayo si salama kwa matumizi ya nyumbani na kusababisha baadhi ya wakazi kuugua homa ya matumbo.
Jamila Omary, mkazi wa kijiji cha Bukene, alisema huduma ya upasuaji ambayo ilikuwa ikisadia mama wajazito haitolewi katika kituo hicho kutokana na ukosefu wa maji.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakihangaika kutafuta huduma hiyo katika hospital ya wilaya ya Nzega huku wale wenye vipato vya chini wakiuza baadhi ya samani zao za ndani ili kupata fedha za usafiri kuifuta huduma hiyo mbal
No comments:
Post a Comment