WAfanyakazi wakiwa kazini kuratibu shughuli hiyo ya maboresho ya rasimu ya huduma kwa mteja picha zote na mahmoud ahmad wa Michuzi blog Arusha. ………………………………………………………Na Mahmoud Ahmad -Arusha
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingiza imewataka wakazi wa jiji la Arusha kukaa mkao wa kula kwani wapo katika wakati wa kuboresha huduma zake kwenye kipindi cha miaka miwili na nusu iliyobakia katika uboresha wa miundombinu na utafutaji wa vyanzo vipya vya maji na kuwa tatizo la maji litakuwa historia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa AUWSA Ruth Koya wakati akijibu maswali ya wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Mkutano wa maboresho ya mkataba wa huduma kwa wateja jijini Arusha.
Alisema kuwa kumekuwa na matatizo ya upungufu wa maji kwa mda mrefu na serikali imeliona hilo ndio maana ikatenga kiasi cha tsh,476 bilion za uboreshaji wa huduma mbali mbali za mamlaka hiyo hivyo suala hilo linafanyiwa kazi kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2018 litakapokamilika.
“Tuwe na subra maradi huu kwa sasa una mda wa miezi nane tangia uanze na mkandarasi wa utafutaji wa vyanzo vya maji yupo kazi akishakamilisha tutaanza maboresho ya miundombinu yetu ilkuweza kuwafikishia maji kwa wateja wetu wote”alisema Koya
Kwa upande wake kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Afisa tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutehengerwa aliitaka Auwsa kuwabainisha wezi wote wa maji ilikuweza kuwafisha katika mikono ya kisheria kwani suala hilo pia linachangia wananchi kukosa huduma ya maji safi na upotevu wa maji.
Alisema kuwa kumekuwapo na vyanzo vingi vya maji zaidi ya 19 na vingine vimeanzishwa na viwanda ambavyo vimekuwa vikiikosesha Auwsa mapato ikiwemo kiwanda cha A to Z ambacho kimekuwa kikigawa maji bure huku wakitambua kuwa wao hawana mamlaka ya kisheria ya usimamizi wa maji hivyo ni mteja mkubwa mnampoteza kulipa huduma za maji
|
No comments:
Post a Comment