• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    KAMPUNI YA SHANTA GOLD MINING YALIPA FIDIA AWAMU YA KWANZA



    Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemamu akitoa maelekezo ya awali kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwalipa fidia wanufaika wote
    Watendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd wakifanya maandalizi ya malipo hayo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
     Baadhi ya wananchi wakisubiri maandalizi yakamilike ili wakabidhiwe mlungula wao
    Dear Mama Exp ndio ndinga iliyotumika kuwafikisha wananchi hao eneo la tukio la kukabidhiwa cheki za malipo kwa wanufaika wote wa Mradi huo
    Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV Elisante Mkumbo kuhusu mchakato wa malipo utakavyo wanufaisha wananchi kupoitia mradi wa uchimbaji madini ya Dhahabu
    Bi Juliana Kidamwe mkazi wa Kijiji cha Mlumbi akihakiki malipo yake kabla ya kukabidhiwa mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson
    Kushoto ni mwasibu wa Shanta Gold Mining Ltd Caroline na Mwanasheria wa kampuni ya Shanta Gold Mining David Rwechungura wakikagua fomu zote za wanufaika kabla ya kuanza zoezi la kuwapatia cheki wanufaika wote wa Mradi huo
    Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida
    Philbert Rweyemamu akitoa maelekezo kwa wanufaika wote ya namna mchakato mzima utakavyokwenda
    Kizito Ramadhani mkazi wa Kijiji cha Mlumbi akikagua fomu za malipo yake mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson kabla ya malipo
    Kutoka kushoto ni Andrea Mtarim Mwenyekiti wa kijiji cha Kinyamberu, Ramadhani Mkuki Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlumbi, Selemani Hema Mtendaji wa Kijiji cha Mlumbi,na Jumanne Gwaye Mtendaji wa Kata ya Mang’onyi wakifatilia kwa makini zoezi la ulipaji fidia
    Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida
    Philbert Rweyemam na Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson wakisisitiza jambo wakati wakizungumza na wanufaika.
     Wananchi wakisikiliza kwa makini maelezo ya malipo yao
    Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida
    Philbert Rweyemamua akikusanya vitambulisho kwa wananchi waliofika ili kurahisisha zoezi la malipo yao
    Normal
    0
    false
    false
    false
    EN-US
    X-NONE
    X-NONE
    MicrosoftInternetExplorer4
    Wanufaika wakipongezana mara baada ya kukamata cheki zao kwa ajili ya malipo ya fidia
    Na Mathias Canal, Singida
     
    Katika miezi miwili ijayo kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu (Shanta Gold
    Mining  Limited) iliyopo katika kijiji cha Sambaru Kata ya
    Mang’onyi Wilayani Ikungi, Mkoani Singida huenda ikaanza uchimbaji wa
    madini ya dhahabu baada ya kuanza kulipa fidia ya zaidi ya Milioni mia nane
    (800,000,000) wanufaika awamu ya kwanza.
     
    Malipo hayo yamekabidhiwa kwa wahusika ikiwa ni siku tatu tu zimepita tangu Meneja wa Mradi
    huo Philbert Rweyemamu alipotoa ahadi ya kuwalipa mwishoni mwa wiki hii
    ili kupisha shughuli za uchimbaji kuanza.
     
    Wanufaika waliolipwa fedha hizo ni wale ambao wanatokanana na mazoezi mawili ya uthamini
    yaliyofanywa kwenye eneo la mradi kwa ajili ya upanuzi wa kambi.
     
    Hafla ya malipo hayo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
    ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambapo wananchi 39 wamejipatia kitita
    chao huku wengine wakishindwa kufika hivyo watakabidhiwa malipo yao wakati
    watakapoyahitaji.
    Malipo
    hayo yanakamilisha umiliki wa maeneo hayo kwa Kampuni ya Shanta Gold mining kwa
    ajili ya uchimbaji na kuwafanya wananchi hao kupisha mradi wa uchimbaji dhahabu
    pasina kinyongo chochote.
    Akizungumzia
    mchakato huo wa malipo hayo Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya
    Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemamu amesema kuwa umefika
    wakati wa wananchi wa Wilaya ya Ikungi na taifa kwa ujumla kunufaika na mradi
    huo utakaoongeza Wigo ya ajira na mzunguko mkubwa wa pesa utakaotokana na wingi
    wa watu watakaodhuru Mkoani Singida kwa ajili ya shughuli za kazi.
     
    Rweyemamu
    alisema kuwa Mradi huo utakuwa na mahusiano chanya kwa wananchi kwani pamoja na
    kuchelewa kuanza kwa uchimbaji lakini imeshiriki ujenzi wa 
    Kituo cha Polisi Mang’onyi ulioanza mwezi May 2013
    na kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2014 na hatimaye
    kuzinduliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Parseko V. Kone.
     
    Akielezea ujenzi
    wa Kituo hicho Rweyemamu alisema kuwa Kituo hicho kimegharimu kiasi cha
    shilingi milioni mia mbili ishirini na tisa, laki tisa sabini na sita elfu na
    mia mbili thelathini (229,976,230) huku lengola ujenzi huo likiwa ni kwa ajili ya kusogeza
    huduma ya usalama karibu na wananchi.
     
    Naye Mwanasheria wa
    Mradi huo wa uchimbaji Madini ya Dhahabu mkoani Singida David Rwechungura amesema
    kuwa Hadi sasa Shanta imewekeza takribani dola za Marekani milioni ishirini na
    tano hapa Singida yaani bilioni hamsini za fedha za Tanzania na bado gharama za
    kujenga mgodi ambazo hazitapungua dola milioni mia moja.
     
    Alisema Mgodi wa Shanta huko Chunya Mkoani Mbeya unazalisha
    takribani kilo 2700 za dhahabu kwa mwaka ambapo pia umetoa ajira kwa
    wafanyakazi 800, licha ya wale ambao wanafaidika kwa kuuza vyakula mgodini na
    kadhalika.
     
    Pamoja na kushiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi Mang’onyi, lakini pia Kampuni ya Shanta
    imeanzisha 
    Mradi
    wa maji  kijiji cha Mangonyi (Kisima
    kimoja kirefu kina meta 60, miundombinu ya kusambaza maji yenye urefu wa
    kilomita 1.3, injini na pampu ya kusukuma maji kwenda kwenye tenki la kijiji na
    polisi
    , imechangia Madawati 100,
    sawia na Samani (yaani vifaa vya ofisi) ya Kijiji hicho.
     
    Naye Mkuu
    wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
    Mtaturu ameipongeza Kampuni ya Shanta kwa kutekeleza ahadi yao kwa wakati
    kwa kuanza kuwalipa wananchi hao fedha zao za fidia kwa wamiliki wa mashamba
    zaidi ya 130 ambapo zaidi ya watu 85 ndio watakaonufaika  na kuifanya leseni ya kampuni hiyo itaanza
    kufanya kazi.
     
    Dc Mtaturu amesisitiza agizo lake alilolitoa la
    kuitaka Kampuni hiyo kuwalipa fidia wananchi 69 wakati wa kikao cha pamoja
    kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Wananchi
    wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi 
    ambacho
    kilipewa jukumu la kuhakikisha wananchi wote ambao watapitiwa na mradi huo
    wanalipwa fidia sambamba na kusimamia uhamishaji wa makazi.
     

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI