• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 26 September 2016

    Katibu Mkuu Aipongeza Muhimbili


    mpok1
    Katibu Mkuu wa Wizara ya AfyaMaendeleo ya JamiiJinsiaWazee na Watoto DkMpoki Ulisubisya(wa pili kushoto) akipewa maelezo kutoka kwa Sista Edeline Jacob baada ya Dk Ulisubisya kuitembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) LEO. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru na kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari Kambi.
    mpok2
    Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Ulisubisya akiwa kwenye wodi mpya wakati alipoitembelea hospitali hiyo leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru na katikati ni  Mkurugenzi wa Ufundi, Mhandisi Gaudence Aksante.
    mpok3
    Mmoja wa wauguzi katika hospitali hiyo akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Ulisubisya wakati alipotembelea Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili leo.
    mpok4
    Mkurugenzi wa Tiba, Dk Hedwiga Swai wa hospitali ya Muhimbili,Mkurugenzi wa Tiba Dk Magreth Mhando kutoka wizara afya na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi wakitoka katika idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili baada ya katibu mkuu kuitembelea idara hiyo leo.
    mpok5
    Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akiwaeleza wageni wa Wizara ya afya jinsi mashine ya CT scan inavyofanya kazi.
    mpok6
    Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Ulisubisya. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari Kambi na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali MUHAS, Henry Sawe.
    ……………………………………………………………..
    Na Neema Mwangomo
    Katibu Mkuu  Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki  Ulisubisya ameupongeza Uongozi wa Hospitali  ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa  kupanua  maeneo ya kutolea huduma za afya.
    Dkt. Ulisubisya ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hospitali hiyo ambako ameona shughuli mbalimbali za maendeleo na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo.
    “ Nimefarijika sana na utendaji kazi wenu kwa kweli mnastahili pongezi  na muendelee kufanya kazi,  kwani asiyefanya kazi hapa si mahali pake,”amesema Katibu Mkuu Dkt Ulisubisya.
    Baadhi  ya maeneo ambayo yanapanuliwa  kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za afya ni Sewahaji Wadi 18,Idara ya Magonjwa ya Dharura na ICU Wadi moja , wadi ambayo tayari inafanya kazi hivi sasa.
    Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru amemuhakikishia Katibu Mkuu kwamba MNH itaendelea kutoa huduma bora na za kibingwa ili Watanzania wanunufaike na huduma zinazotolewa na hospitali hiyo.
    “Mpango uliopo ni kuhakikisha MNH inaonyesha njia na kuwa mfano, tutafanya kila tuwezalo ili kutatua changamoto zilizopo ili kuendana na dira ya serikali,” amesema Profesa Museru.
    Maeneo aliyotembelea ni Mwaisela ICU Wadi Moja, wadi tatu, Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Idara ya Radiolojia, Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Wadi 18 Sewahaji , Maabara Kuu na jengo la Watoto

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI