
Viongozi wa serikali na Jeshi la polisi wakipata maelezo jinsi huduma zinavyotolewa katika Zahanati Mwendo

Viongozi wa serikali na Jeshi la polisi wakipata maelezo jinsi huduma zinavyotolewa katika Zahanati Mwendo

Madereva wakipima afya zao
Mwonekano wa Zahanati Mwendo kwa nje
……………………………………………………………….
-Wananchi wapata mafunzo ya unywaji kistaarabu
Huduma ya Zahanati Mwendo ambayo imebuniwa na kampuni ya TBL Group katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani kwa ajili ya kupima afya za madereva imekuwa kivutio kikubwa mkoani Geita ambako maadhimisho haya yamezinduliwa kitaifa na idadi kubwa ya madereva na wananchi wanaendelea kujitokeza kupima afya zao kwa wingi na kupatiwa matibabu na ushauri nasaha.
Madaktari maalumu waliopo kwenye gari la kufanyia vipimo la Zahanati Mwendo muda wote tangia kuwasili mkoani Geita wamekuwa na kazi kubwa ya kutoa huduma kwa madereva wengi na wanaendelea kujitokeza kufanyiwa vipimo siku hadi siku.
Meneja Mawasiliano wa TBL Group ,Amanda Walter,amesema inavutia kuona watanzania wengi wanahitaji huduma ya kupimwa afya na kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa madereva na wananchi wanaotembelea Zahanati Mwendo.
Alisema pia kuwa wananchi wengi wamejitokeza katika semina ya Mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu yaliyofanyika katika kituo Kikuu cha mabasi cha Geita ambapo walipata fursa ya kujua madhara ya matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kupindukia.
”Wiki ya Usalama ya mwaka huu imekuwa na mwamko mkubwa hususani wananchi walivyojitokeza kwa wingi katika mafunzo haya ya Unywaji wa Kistaarabu na mengine yanayohusina na Usalama barabarani.TBL Group tunaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kampeni za Usalama kwa lengo la kupunguza matukio ya ajali nchini”Alisema.
Rehema Nyoki,mkazi wa Geita ambaye amehudhuria mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu akiongea kwa niaba ya wenzake aliipongeza kampuni ya TBL Group kwa kuendesha semina za uhamasishaji unywaji kistaarabu na alitoa ombi mafunzo hayo yafikishwe sehemu mbalimbali nchini kwa kuwa ipo idadi ya waathirika wengi wa kutumia vinywaji vyenye kilevi kupita kiasi kwenye jamii ambao wanaishia kupata matatizo ya kila aina.
No comments:
Post a Comment