MAHAKAMA ZASHAURIWA KUZINGITIA HAKI

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (kulia) wakati wa hafla ya kumuga Jaji huyo iliyofanyika katika ukumbi namba moja wa Mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Shaban Ali Lila, Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kuagwa kwake leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na. . Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya kuagwa kwa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo leo Jijini Dar es Salaam.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo akipongezwa na mototo wake wa kike, Bi. Noera Kileo wakati wa hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama Kuu, leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (watatu kutoka kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (kulia) wakati wa hafla ya kumuga Jaji huyo leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama.
Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.
…………………………………………………………
Na.Sheila Simba-Maelezo
Mahakama nchini zimetakiwa kuzingatia haki ya msingi katika kutenda kazi,kuliko ufundi wa kisheria unaotumiwa na wanasheria katika kufanya kazi zao za kila siku.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Jaji Angera Kileo katika hotuba yake wakati wa hafla ya kumuanga iliyofanyika katika ofisi za Mahakama Kuu.
Amesema kuwa ni vyema haki itendeke kwa kila mtu ili kusaidia jamii kupata haki pale wanapokua na tatizo na kuongeza kuwa ni imani yake kuwa mwenye mamlaka ya kutoa uhai ni yule alikupa uhai pekee.
“Watoaji haki sio wote wamekamilika tunapoamua kutoa hukumu ya kifo unaweza kutoa kwa mtu ambaye hakutenda kosa hilo na kumuacha aliyefanya kosa”alisema Jaji Kileo
Aidha,ameeleza kuwa mahakama zinahitaji kusaidiwa katika kazi zake za uendeshaji wa kesi kwani ni gharama na wakati mwingine mahakama zinashindwa kutimiza wajibu wake kutokana na kushindwa kumudu gharama.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othmani Chande, akizungumzia wasifu Jaji Kileo amesema mahakama uadilifu na uaminifu wa Jaji huyo katika kipindi cha miaka 40 aliyoitumia sekta ya sheria nchini.
“kwa kweli Jaji Kileo amefanya kazi kubwa na anaondoka akiwa ametuachia urithi mzuri hasa wa kutumikia haki ya msingi katika kutenda haki na sio kuangalia ufundi wa kisheria kama ambavyo alivyokuwa anafanya kazi” alisema Chande
Ameongeza kuwa Jaji Kileo alikuwa ni mtu wa kuhakikisha kila mtu anapata haki yake na kuheshimu haki na kusiitiza majaji wanawake kuiga mfano wake ili kusaidia mahakama kufanya kazi zake kwa kuzingatia maadili ya kazi.
No comments:
Post a Comment