Ibada ya mwaka huu imekuwa ya mafanikio kwa kumalizika salama, hii ni kutokana na Serikali ya Saudi Arabia kuwa na mipango madhubuti kwa kuimarisha miundombinu, usafiri, ulinzi na usalama na kurekebisha dosari zilizojitokeza mwaka jana.
Maeneo ya misikiti yote miwili ya Makkah na Madina yaliimarishwa na yanaendelea kujengwa ikiwa ni pamoja na kupanuliwa ili kuongeza nafasi za kutosha kufanyia ibada.
Mahujaji kutoka Tanzania wapatao 2,000 wako salama na wao ni miongoni mwa walioshiriki katika ibada na sasa wako njiani kurejea Tanzania. Hatua zilizochukuliwa na mamlaka za ulinzi za Saudi Arabia ni pamoja na kuhakikisha kuwa makundi ya misafara ya mahujaji hayagongani kati ya wanaokwenda na wanaorudi, njia mbalimbali zilikuwa zikifungwa na kufunguliwa ili kuruhusu misafara kwenda uelekeo mmoja bila kukutana. Hatua hii ilisaidia kuepusha ajali kama iliyotokea wakati wa ibada ya hijja ya mwaka 2015.
Habari hizi ni kwa mujibu wa Kamati ya Hijja ya Tanzania
No comments:
Post a Comment