• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 23 September 2016

    MCHELE NA MAFUTA YA KULA VYAKAMATWA NA IDARA YA BIASHARA PEMBA

    indexNa Masanja Mabula -Pemba ..
    JUMLA ya pakti 23 za mchele pamoja na dumu 31 za mafuta ya kula yenye ujazo wa lita ishirini (20) zimekamatwa na Idara ya Biashara Pemba yakiwa katika harakati za kusafirishwa kwenda nje ya Kisiwa cha njia ya magendo .
    Bidhaa hizo zilikuwa na maafisa wa Idara ya Biashara zikiwa zimepakiwa ndani ya mashuwa ambayo ilikuwa inaekelea Mkoa wa Tanga katika eneo la bandari bubu iliyoko Mtambwe Mkuu shehia ya Mtambwe Kaskazini Wilaya ya Wete.
    Akizungumzana watendaji wa Wizara ya Biashara , Viwanda na Masoko Pemba , Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman aliwataka kuendelea kusimamia haki na kuwataka kutomuonea mtu kutokana na imani ya chama chake .
    Aidha alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Wete , kumtafuta mfanyabiashara aliyekuwa anasafirisha bidhaa hivyo na kuhakikisha anafikishwa mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua za kisheria .
    “Mkuu wa Wilaya nakuomba utumie uwezo uliopewa kisheria kumtafuta mfanyabiashara huyu ambaye alikuwa analengo la kukwepa ushuru na akipatikana awekwe ndani ya muda wa masaa ishirni (24)  ulioyopewa na sheria ” alifahamisha.
    Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali akizungumzia tukio hilo , amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wa Serikali pamoja na vyombo vya ulinzi kuimarisha ulinzi na doria katika maeneo yote ya bandari bubu ili kudhibiti biashara ya magendo .
    Alisema kupitia kamati ya ulinzi na usalama , wamejipanga kuzidhibiti bandari bubu ambazo zimekuwa zikitumiwa na wahujumu wa uchumi kupitisha bidhaa zao kinyume na sheria na bila ya kulipa kodi .
    Kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Biashara , Viwanda na Masoko Pemba Abdalla Juma Khamis alisema , Serikali haijazuia wananchi kusafirisha mchele kwenda nchi ya Kisiwa lakini kinachotakiwa ni mfanyabiashara kulipa kodi na kupatiwa risiti halali .
    Alifahamisha kuwa , pamoja na fursa hiyo lakini bado baadhi ya wananchi wanaendelea kwenda kinyume na taratibu hizo na hivyo kuikosesha mapato Serikali .
    “Tumepokea simu muda mfupi uliopita kwamba mfanyabiashara aliyekuwa anahusika na mchele huo atakuja kesho ofisini , lakini sheria zipo , itabidi alipe gharama zaote zilizotumika kusafirisha bidhaa hii hadi hadi hapa , kulipa faini pamoja na kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na mzigo atarejeshewa mwenyewe  ” alifahamisha.
    Mkuu wa Idara ya Biashara Pemba , Ali Suleiman Abeid alisema kwamba taarifa ya kutaka kusafirishwa kwa  bidhaa hizo walizipata kutoka kwa raia wema , na hivyo kufanikiwa kuzima jaribio hilo 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI