• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO, MHANDISI FELCHESMI MRAMBA ATEMBELEA BUKOBA KUTATHMINI ATHARI ZA TETEMEKO


     Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (wapili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika hilo mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, (kulia), wakati alipotembelea kituo cha 
    Kabeta
     Wateja wakiwa wamepanga foleni kupata huduma za umeme kwenye kontena lililowekwa nje ya ofisi za Shirika hilo mkoani Kagera, baada ya jengo hilo kuathirika vibaya
    /* Style Definitions */
    table.MsoNormalTable
    {mso-style-name:”Table Normal”;
    mso-tstyle-rowband-size:0;
    mso-tstyle-colband-size:0;
    mso-style-noshow:yes;
    mso-style-priority:99;
    mso-style-qformat:yes;
    mso-style-parent:””;
    mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
    mso-para-margin-top:0in;
    mso-para-margin-right:0in;
    mso-para-margin-bottom:10.0pt;
    mso-para-margin-left:0in;
    line-height:115%;
    mso-pagination:widow-orphan;
    font-size:11.0pt;
    font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
    mso-ascii-font-family:Calibri;
    mso-ascii-theme-font:minor-latin;
    mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
    mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
    mso-hansi-font-family:Calibri;
    mso-hansi-theme-font:minor-latin;}
     NA K-VIS BLOG/Khalfan
    Said, Bukoba
    MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika
    la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, amekagua miundombinu
    ya Shirika hilo iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi na kuzungumza na wafanyakazi
    mjini Bukoba mkoani Kagera leo Septemba 16, 2016.
    Karibu jengo lote la
    Ofisi za makao makuu ya TANESCO, limepata nyufa nyingi na hivyo kuufanya
    uongozi wa Shirika hilo mkoani Kagera, kuhamishia shughuli zake nje ya jengo,
    ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wateja kwenye makontena mawili ambayo yamewekwa
    nje ya Ofisi hizo.
    Mhandisi Mramba ambaye
    amewasili mjini Bukoba mapema leo asubuhi Septemba 16, alianza ziara yake kwa
    kukagua vituo vya kupoozea na kusambaza umeme vya Kabeta, Kyaka na Misenyi na
    kuzungumza na wafanyakazi.
    “Nianze kwa kuwapongeza
    wafanyakazi wenzangu kwa hatua za haraka mlizochukua mara baada ya kutokea
    tetemeko la ardhi, kwa kuhakikisha mnazima umeme, hiyo imepelekea kuepusha vifo
    ambavyo vingesababishwa na umeme wakati wa tetemeko hilo,” Alisema Mhandisi
    Mramba, wakati akiongea na wafanyakazi nje ya jengo la makao makuu ya TANESCO
    mkoani Kagera.
    Mhandisi Mramba, pia
    alisema, “Baada ya kukagua vituo vyetu vya kupooza na kusambaza umeme,
    tunashukuru Mungu, hakuna athari katika mifumo yetu ingawa majengo yamepata
    nyufa na mengine yanahitaji kufanyiwa ukarabati wa haraka,” alsiema.
    Mhandisi Mramba pia
    aliwataka wafanyakazi wa TANESO, kuwasaidia wenzao waliopatwa na athari
    kutokana na tetemeko hilo ambapo yeye mwenyewe alianzisha harambee na
    kufanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 3.3 zikiwemo fedha taslimu na
    ahadi zilichangwa.
    “Sisi kama shirika
    tumekwisha toa mchango wetu wa jumla kusaidia waathirika wa tetemeko hili
    kupitia Msajili wa Hazina, lakini kwa vile waathirika wa tetemeko hili ni
    watanzania wenzetu, ni wadau wetu wakubwa, nimeagiza ofisi zetu kote nchini
    kuzungumza na wafanyakazi ili tufanye mchango kuwasaidia watanzania wenzetu.”
    Alisema.
    Naye Meneja wa TANESCO
    mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, aliwapongeza wafanyakazi wa wake kwa
    kufanya kazi kubwa katika kipindi chote tangu janga hilo litokee, na kuwataka
    waendelee kulitumikia taifa kwa moyo wa kizalendo na upendo.
    Watu 17 walipoteza
    maisha, huku wengine zaidi ya 200 wakijeruhiwa na  nyumba zaidi ya 5,000 zikiharibiwa na
    tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha Richa 5.7 na lililotikisa umbali wa
    kilomita 10 chini ya ardhi. Tetemeko hilo lilitokea majoira ya jioni ya
    Septemba 10, 2016.
     Mhansisi Mramba akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea kituo cha Kabeta
     Mhandisi Francis Maze
    Mwangalizi msaidizi wa ofisi za Kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Misenyi
     Mhandisi Mramba, akikagua athari za tetemeko kwenye makao makuu ya TANESCO mkoani Kagera
     Mhandisi Mramba, na ujumbe wake wakitembelea kituo cha Misenyi
     Mhandisi Mramba (kushoto), akizungumza na wafanyakazi
     Mfanyakazi wa TANESCO mkoani kagera ambaye nyumba yake iliathirika akizungumza kwenye mkuytano huo
     Wafanyakazi wa TANESCO mkoani Kagera
    Hili ndilo jengo linalotumiwa na TANESCO kama makao makuu yake mkoani Kagera, ambalo limepata nyufa nyingi na kupelekea huduma za umeme kwa wateja kutolewa nje ya jengo hilo ambapo wateja wanaonekana wakiwa kwenye foleni

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI