• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 4 September 2016

    Vijana 7,170 waliopitia JKT waajiriwa



    VIJANA 7,170 waliojiunga kwa kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wameajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama kuanzia mwaka 2010 mpaka sasa.
    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Ali Mwinyi alisema kuanzia mwaka huo, JKT huchukua vijana 5,000 hadi 7,000 kwa madhumuni ya kuwapa stadi za kazi na kuwajengea uzalendo.
    Akizungumza katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Televisheni ya Shirika la Utangazaji Taifa (TBC1), Dk Mwinyi alisema kuanzia mwaka 2010 vyombo vya ulinzi na usalama viliacha kuajiri kutoka uraiani, bali vijana waliopitia mafunzo hayo ambapo zaidi ya vijana 2,000 wamekuwa wakiajiriwa kwa mwaka.
    Alisema pia kwa sasa kuna taasisi nyingi zimeanza kuchukua vijana waliopitia mafunzo hayo kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) na kampuni binafsi za ulinzi.
    “Wakati wa kuwachukua tunawaeleza mapema kuwa yale ni mafunzo na si ajira na wapo watakaobaki baada ya vyombo vyote kuajiri hivyo kutumia stadi za kazi walizofundishwa kujiajiri na sasa kuna mipango ya kuwawezesha kutumia ujuzi waliopata,” alisema Dk Mwinyi.
    Akizungumzia kuhusu tuhuma za vijana wasiopata ajira baada ya mafunzo ya JKT kujiingiza katika vitendo vya uhalifu, alisema hayo ni maneno ya mitaani na hayajathibitishwa.
    “Hili jambo halijathibitishwa na siamini kama hili linawezekana kwani pamoja na kupewa mafunzo ya kijeshi, lakini wanapewa mafunzo ya uzalendo na nadhani wanakuwa wazalendo kuliko ambao hawajapita JKT. Lakini kabla halijathibitishwa hatuwezi kusema kwa uhakika, lakini nina imani wanakuwa wamepikwa na kuweza kujiajiri,” alieleza. Alisema ili kujiunga na mafunzo ya kujitolea, JKT hufanya usaili wilayani na mikoani na hakuna utaratibu mwingine.
    Alitoa onyo kwa watu binafsi wanaodanganya watu kusaidia vijana kujiunga na JKT.
    Dk Mwinyi alisema mwaka huu wanajeshi wa kujitolea wamechelewa kwenda kambini kutokana na uhaba wa fedha za bajeti, hivyo watakapopata fedha kutoka Hazina kwa ajili ya sare na vyakula watawaita waliochaguliwa kuanza mafunzo kwa kutoa taarifa rasmi.
    Kuhusu uwiano kati ya wanawake na wanaume jeshini, alisema huwa wanatoa kipaumbele kwa wanawake kwa kuwa kihistoria jeshi ni la wanaume sasa wanataka kubadilisha kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake kwa kuongeza idadi ya wanawake kufikia asilimia 20

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI