• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 5 September 2016

    WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI KUSHIRIKI UANGALIZI WA UCHAGUZI WA WABUNGE KATIKA JAMHURI YA SHELISHELI.

    Mahiga
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Alix Michel.
     
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akimtambulisha Balozi Innocent Shiyo kwa Rais wa Shelisheli, Alix Michel
    Rais wa Shelisheli, Alix Michel akiwa kwenye kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Baloz Dk. Augustine Mahiga nchini Shelisheli.
     
    Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha ya
    pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
    Balozi Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani
    ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
    ………………………………………………………………………………………
     
    Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama
    ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ), katika Mkutano wa 36
    wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31
    Agosti, 2016. 
    Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8
    – 10 Septemba, 2016.
    Wajibu huu wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi imetokana na
    misingi na muongozo wa chaguzi za kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa chini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga (Mb), alizindua  rasmi misheni hiyo tarehe 2 Septemba, 2016 kwa
    niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya waangalizi itakua na
    waangalizi kutoka nchi  za SADC .
     
    Wakati akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga alipata fursa ya kukutana na
    kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix  Michel Rais wa Sheliseli . 
     Pia Mheshimia Waziri Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel Morgan,  Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychels na kukutana  na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Seychels.

    Imetolewa na :
    BALOZI  INNOCENT E. SHIYO

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI