• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    WEKEZENI KATIKA KILIMO NA MADINI ILI KUFIKIA UCHUMI


    Wito huo umetolewa na Profesa Haji Semboja katika mahojiano na MAELEZO kuhusu hali ya uchumi nchini katika kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
    “Muhimu sasa Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya Madini,kilimo na viwanda na hili litasaidia kufanya nchi kuzalisha bidhaa zitakazouzwa nchini kwa wingi bila kutengemea bidhaa kutoka nje ya nchi”,alisema Prof.Semboja.
    Ameeleza kuwa taarifa ya hali ya uchumi iliyotolewa na Benki Kuu nchini imeweka wazi hali ilivyo kwa sasa,na kuongeza kuwa ni kweli uchumi upo imara kutokana na taarifa zilizokusanywa na Benki  hiyo kutoka vyanzo mbali mbali.
    “Ni kweli kwamba uchumi wetu upo imara na kwamba uchumi wetu unapimwa kwa kuangalia vigezo vinne ambavyo  ni pato la taifa,mfumuko wa bei,urari wa biashara na upungufu wa fedha serikalini”,alisema Prof. Semboja.
    Aidha,Prof Semboja amesema kuwa serikali kwa sasa imepunguza matumizi ya fedha yasiyo ya lazima na imeongeza makusanyo ya kodi 
     
    Na Sheila Simba,Maelezo
    ………..
    Serikali meshauriwa kusimamia uwekezaji  katika sekta za kilimo,madini na viwanda ili kufikia malengo waliojiwekea ya kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.kutoka vyanzo mbalimbali.  
    “Serikali haina matumizi makubwa ya fedha kwani matumizi yanendana na mapato yanayokusanywa ”,alisema Semboja
    Amesema kuwa wanaolalamikia kutoonekana kwa fedha mtaani ni wale waliokuwa wanapata pesa kwa njia ambazo sio halali na hivyo kupelekea kushindwa kupata kwa sasa kutokana na udhibiti uliwekwa na Serikali katika kukusanya na kusimamia kodi kwa utaratibu halali.
    Ameongeza kuwa Serikali fedha inazokusanya zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote na sio kwa wachache waliokuwa wakijinufaisha wenyewe.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI