• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 21 September 2016

    Yanga haitoki Kambarage



    TIMU ya soka ya Stand United ya Shinyanga imetoa tahadhari kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga kwamba wasitarajie mteremko katika mechi yao itakayochezwa keshokutwa.
    Stand inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Yanga kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga, Jumapili, ikiwa ni mechi muhimu kwa timu zote kupata pointi tatuy.
    Jeuri hiyo ya Stand imekuja baada ya kushinda bao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
    Kwa upande wa Yanga ambayo ipo Shinyanga tangu wiki iliyopita, ilicheza na Mwadui na kuishinda mabao 2-0.
    Akizungumza na gazeti hili, kocha msaidizi wa Stand, Athuman Bilal alisema timu yake kwa sasa imeingia kambini katika wilaya ya Kahama kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Yanga. Kocha Bilali alisema Yanga ni timu ya kawaida na anazishangaa timu zote zinazofungwa na Yanga.
    “Yanga ni timu ya kawaida kabisa nimewaona wakicheza na Mwadui ile wikiendi iliyopita, Yanga beki zao hazijatulia bado zinafanya makosa mengi nitahakikisha tunawafunga hapa nyumbani kwetu na tukirudiana nao tunawafunga tena kwao,” alisema.
    Bilal alisema ana imani kubwa na safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Kelvin Kongwe, Suleiman Selembe, Jeremiah Katula na Amri Kiemba.
    “Safari hii tunajizatiti kuhakikisha kwamba hata tusipoongoza kwenye ligi, basi angalau tuwe katka nafasi ya kuridhisha ikiliganishwa na msimu uliopita,” Bilal.
    Stand United mpaka sasa ipo katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi tisa huku Yanga ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 10.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI