Dar es Salaam Oktoba 28, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, alisema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.
“Tunawashukuru wateja wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na wadau wote ambao kimsingi wametusaidia na kuwa nasi katika safari yetu hii ya mafaniko,” alisema Weesie.
Bia ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na vionjo vya hapa nchinikupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza.
Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.
“Tunaona fahari kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager katika ubora uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi kutokana na kutambuliwa na wateja wetu wa ndani pamoja na medali zaidi ya 10 za kutambulika kimataifa ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba tutaendeleakuzalisha Serengeti Premium Lager katika ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema Weesie.
Uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Serengeti pia umekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” Aidha kampuni hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996.Anayefuatia katikati ni Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi na mwishoni kulia ni Mkurungezi mkuu wa SBL Helene Weesie.Mkutano huu umefanyika mapema jana katika Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.
Mpishi Mkuu mtanzania Winston Kagusa aliyefanikiwa kuchanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na vionjo vya hapa nchini kupata kinywaji hiki cha Serengeti Premium Lager kinachopendwa na wengi.
Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akiongoza katika kuzindua chapa mpya ya Serengeti Premium Lager sherehe ambazo zinaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya bia hiyo kulia kwake ni Meneja Masoko wa SBL Anitha na kushoto kwake wa kwanza ni Mpishi Mkuu wa kwanza wa Serengeti Premium Lager Winston kagusa na mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko Cesear Mloka.Hafla hii ilifanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano, SBL John Wanyacha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika Mkutano wa waandishi wa habari ambapo Bia ya serengeti premium lager inatimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake na pia kuzinduliwa kwa chapa yenye muonekano mpya.Mkutano huu ulifanyika mapema jana katika hotel ya Hyatt Regency
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment