• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday 30 October 2016

    BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU YATANGAZA WANAFUNZI 5,326 KUPATIWA MIKOPO KARIBUNI


     Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, (HELSB), Abdul-Razaq Badru, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo, jijini Dar es Salaam, Oktoba 30, 2016
    Bw. Badru, (kulia), akiongozana na Afisa Habari wa HELSB, Omega Ngole kuingia ukumbi wa MAELEZO

    NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
    BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini, (HELSB), imesema kwa sasa inakamilisha upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 5,326 walioomba mikopo kwa muhula wa masomo 2016/2017 ili kufikia lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi 25,717.
    Hayo yamesemwa leo Oktoba 30, 2016 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini, (HELSB), Bw. Abdul-Razaq Badru, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu vigezo vya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017, mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.
    “Tayari tumekwishatoa mikopo kwa wanafunzi 20,391 kati ya wanafunzi 25,717 wa mwaka wa kwanza ambao ndio wamefikia vigenzo vya kupewa mikopo kwa mwaka huu wa masomo 2016/2017.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB.
    Alirejea kusema kuwa upangaji huo wa mikopo umezingatia vigezo vilivyowekwa na serikali ambavyo ni pamoja na Uyatima na ulemavu,uhitaji wa waombaji katika familia zenye hali duni ya kimaisha hususan waliosoma katika shule za umma, lakini pia vipaumbele vya kitaifa vinavyoendana na mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 20125 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele kama vile,
    1)  Fani za Sayansi
    2)  Ualimu wa Sayansi na Hisabati
    3)  Uhanisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asili
    4)  Sayansi Asilia
    5)  Sayansi za ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
    Akitoa takwi mu za makundi ya wanafunzi waliopengiwa mikopo, Mkurugenzi huyo Mtendaji wa HELSB amesema, upangaji wa mikopo 2016/2017 ulizingatia bajeti ya shilingi bilioni 483 iliyopitishwa na Bunge kwa ajili ya kuwakopesha jumla ya wanafunzi 119,012 kati ya wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 93,295 ni wale wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali nchini.
    Hata hivyo, Bw. Razaq Bdru, alisema idadi ya wanafunzi walioomba mikopo mwaka huu wa masomo na wenye sifa stahiki ni 30,957 ambao wameingizwa kwenye mfumo wa kuchakata na kupanga mikopo kwa mujibu wa sifa zao na vigezo vilivyowekwa.
    “Katikati ya wiki ijayo tutachapisha orodha  ya wanafunzi 5,326 waliosalia kupata mikopo.” Alitoa hakikisho.











     Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Dar es Salaam, Edson Mwakyombe, akiwa na huzuni baada ya kusikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB. Kijana huyu anayechukua shahada ya ualimu ni yatima na amekosa mkopo awamu ya kwanza

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI