• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 28 October 2016

    MADEREVA WA FUSO ZA MICHANGA WAANDAMANA LEO KIBAHA


    Madereva wa magari ya michanga kibaha wameilalamikia serikali ,  baada ya kukamatwa magari 10 na Tanrod, Kwa tuhuma za kutofunika magari maturubai. Lakini madereva hao walikataa na kusema kuwa magari yetu tunayafunika. Tunashindwa kuwaelewa Tanrod wanachokitaka kwetu ni nini? Maana sheria zote tumezitimiza na magari tunayafunika.


    Baada ya hapo Z4 News ilipata kuongea na mmoja wa wamiliki wa magari hayo, Akasema kuwa  tatizo lililopo kubwa mpaka sasa hatujaelewa maana sheria zote tumezitimiza. Tunashangaa leo hii tunapewa kesi ambazo hazieleweki na kama gari itafungwa mchanga utatokea wapi? Kiukweli tunashindwa kuelewa kuwa Tanrod malengo yao yapo wapi.


    Hata hivyo wananchi hao waliendelea kupiga kelele na faini hiyo kubwa wanayotozwa kiasi cha shilingi laki tano.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI